Ameiambia serikali ya kiraia kwamba hakuna vizingiti vyovyote katika kujihusisha kwenye mazungumzo na adui.
Matamshi ya Ayatollah Ali Khamenei yanaweka wazi masharti kwa mazungumzo yanayoweza kufanyika chini ya utawala wa rais mpenda mageuzi Masoud Pezeshkian, na pia kuelezea tena maonyo yake kwamba Marekani si nchi ya kuaminika.
Lakini maoni yake yanazingatia wakati kulipokuwa na makubaliano na Iran mwaka 2015 kuhusu mpango wake wa nyuklia, yaliyohusisha nchi nyingine zenye nguvu duniani.
Makubaliano hayo yalipelekea uwezo wa Iran kutengeneza nyuklia kupunguzwa kwa kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.
Khamenei, mwenye umri wa miaka 85 uamuzi wake ni wa mwisho katika maswala ya Iran, amesema kwamba Iran haistahili kuweka tumaini lake kwa adui na si lazima kutekeleza makubaliano ya adui ili kuendelea na mipango yake, akionya baraza la mawaziri la Pezeshkia kwamba lisiwaamini maadui.
Rais wa zamani Donald Trump, aliiondoa Marekani kwenye mkataba na Iran kuhusu nyuklia.
Baadhi ya taarifa katika habari inatokana na vyanzo mbalimbali
Forum