Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 02:08

WHO haijakaribishwa kuungana na wachunguzi wa janga la corona China


Dkt. Gauden Galea

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Alhamisi kuwa halijapata mwaliko kutoka China kuungana na wachunguzi wanaotafuta chanzo cha janga la virusi vya corona.

Mwakilishi wa WHO mjini Beijing Dkt Gauden Galea amesema alitarajia China itazungumzia ushirikiano na taasisi hiyo katika “siku za karibuni.”

“Tunajua kuwa baadhi ya uchunguzi unafanyika lakini katika hatua hii hatujakaribishwa kushiriki. Tunatarajia, siku za karibuni, kupewa muhtasari hilo litafanyika wapi na kujadili uwezekano wa kushirikiana nao,” ameseme Galea.

Ugonjwa wa virusi vya corona COVID-19, ambao uliibuka katika mji wa Wuhan nchini China, umeuwa watu zaidi ya 230,000 duniani, kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, na kuthibitisha kuwa maambukizi yamefikia watu milioni 3.2.

Beijing imekosolewa kwa ukosefu wa uwazi katika kukabiliana na janga hili, wakati Marekani ikifanya uchunguzi iwapo virusi hivyo vilitokana na maabara ya uchunguzi wa kutafuta kinga dhidi ya maambukizi ya virusi vinavyo wadhuru binadamu na wanyama.

Idadi ya rasmi ya maambukizi iliyotolewa Wuhan imekuwa ikihojiwa tangu mwanzoni ambapo serikali ya China mara kwa mara ilikuwa inabadilisha vigezo vya hisabu hiyo wakati maambukizi yalipofikia kileleni.

Wakati huohuo China imetupilia mbali uwezekano kwamba janga la virusi vya corona lilianzia katika maabara hiyo na kuwa haijatokana na maambukizi ya wanyama kwa wanadamu huko Wuhan kama inavyoaminika hivi sasa.

Hata hivyo asili ya COVID-19 bado haijajulikana, baadhi ya wanasayansi wanashuku kuwa virusi hivyo viliambukizwa na Wanyama kwa wanadamu katika soko la mazao ya baharini huko Wuhan.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG