Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 27, 2022 Local time: 00:37

China : Hospitali mjini Wuhan zawaruhusu wagonjwa wote wa COVID-19 kuondoka baada ya kupona


Wafanyakazi wa afya wakisheherekea baada ya wagonjwa wote wa COVID-19 kuruhusiwa kutoka hospitali ya muda iliyokuwa ikitoa huduma ya dharura katika jimbo la kati la Hubei Machi 9, 2020. (Photo by STR / AFP) / China OUT

Wagonjwa wote wa COVID-19 wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kuthibitishwa wamepona na kurejea majumbani kwao mjini Wuhan, ambako mlipuko wa virusi hivyo uliibuka nchini China mwisho wa mwaka 2019, maafisa wa nchi hiyo wamesema Jumapili.

Hilo lilipelekea kuenea kwa maambukizi hayo sehemu nyingine duniani. Sehemu nyingi duniani zinatekeleza amri ya kutotoka nje katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya janga hilo la COVID.

WUHAN

Vyanzo vya habari vimesema maafisa wa afya wa jiji la Wuhan wametangaza kutokuwa na mgonjwa yoyote aliyelazwa hospitalini kutokana na maradhi yanayosambazwa na virusi hivyo.

Kwa mujibu wa afisa wa Tume ya Kitaifa ya Afya, China, Mi Feng ripoti mpya inaonyesha hakuna maambukizi yoyote ya virusi vya corona kwenye jiji hilo, na kupongeza hatua za pamoja kati ya Wuhan na wahudumu wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini humo.

Jiji hilo liliripoti juu ya watu 46,452 waliokuwa wanaougua homa ya mapafu COVID-19 sawa na asilimia 56 ya maambukizi yote nchini China. Watu 3,869 walifariki dunia.

NEW YORK

Wakati huohuo wakazi wa mji wa New York wataweza kuanza kupimwa katika maduka ya dawa yaliyoko karibu na maeneo yao wanayoishi, Gavana wa New York Andrew Cuomo amesema Jumamosi.

Cuomo amesema maduka ya dawa 5,000 yataruhusiwa kuwapima watu, na lengo ni kufikia vipimo 40,000 kila siku.

Kadhalika wafanyakazi walioko mstari wa mbele katika hospitali nne New York wanaokpambana na ugonjwa huu watapimwa kinga zao dhidi ya virusi, gavana ameeleza.

IDADI YA MAAMBUKIZI

New York ni kitovu cha mlipuka wa virusi vya COVID-19 nchini Marekani. Idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo New York ni takriban theluthi moja ya idadi ya vifo 54,000 vilivyotokea hadi hivi sasa kutokana na maradhi haya nchini Marekani.

WHO

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha Jumamosi kuwa “hakuna ushahidi” kwamba wale waliopona kutokana na COVID-19 na wanakinga tayari mwilini dhidi ya ugonjwa huo hawawezi kuambukizwa virusi vya corona kwa mara nyingine.

WHO imetoa tahadhari hiyo katika maelezo yake ya kisayansi wakati ikithibitisha maambukizi ya virusi vya corona duniani kufikia milioni 2.8.

CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS

Vifo katika nchi mbalimbali duniani vimevuka 200,000, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins kilichoko Jimbo la Maryland. Mapema Jumapili Johns Hopkins ilisema jumla ya vifo duniani kutokana na COVID-19 imefikia 203,043.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG