Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 04:22

COVID-19 : UNICEF yahamasisha msaada kwa ajili ya Mashariki ya Kati, Afrika Kaskazini


Kijana aliyekimbia vita huko Mosul, akipatiwa chanjo ya suruwa kutoka kwa mfanyakazi wa afya anayesaidiwa na shirka la UNICEF katika mji wa Hamdaniyah, Iraqi Oct. 24, 2016.
Kijana aliyekimbia vita huko Mosul, akipatiwa chanjo ya suruwa kutoka kwa mfanyakazi wa afya anayesaidiwa na shirka la UNICEF katika mji wa Hamdaniyah, Iraqi Oct. 24, 2016.

Idadi ya vifo na maambukizi kutokana na ugonjwa unaosababishwa na virusi vipya vya corona COVID-19 inaendelea kuongezeka kote duniani ambapo zaidi ya watu 166,256 wamefariki na 2,432,092 wameambukizwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto, UNICEF, imetoa wito hii leo ikihamasisha msaada zaidi wa karibu dola milioni 92.8 ili kupambana na janga la ugonjwa wa COVID-19 katika nchi za Mashariki ya kati na Afrika kaskazini.

UNICEF inasema kwamba kanda hizo zinazokumbwa na ghasia ndizo zenye watoto wengi zaidi wanaohitaji msaada makubwa kuliko maeneo mengine duniani.

Fedha zaidi zinahitajika ili kugharimia miradi mbali mbali katika kanda hizo ili kupunguza athari za janga la Corona amesema mkuu wa kikanda wa Unicef Ted Chaiban.

Kabla ya janga hilo zaidi ya watoto milioni 25 huko mashariki ya kati na Afrika kaskazini walikuwa wanahitaji msaada kutokana hasa na vita huko Yemen, Syria na Libya.

Marekani imeendelea kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa na vifo, ambapo hadi Jumatatu maambukizi yamefikia 760,570 na vifo ni 40,702.

Wakati huohuo huko Uhispania kumekuwa na ongezeko la vifo mwishoni mwa wiki kupindukia elfu 20, hata hivyo idadi ya watu wepya kuambukizwa nchini humo ilianza kupungua.

Itali kwa upande wake imeshuhudia kupungua kwa watu wanaokufa ambapo watu 433 walifariki kati ya Jumapili na leo. Nchini humo baadhi ya maduka yameanza kufunguliwa pole pole. Wakati Norway inapanga kufungua shule za msingi sawa na mji wa Huan huko china kitovo cha mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG