Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 17:41

Kundi la G-20 laendelea kuchangisha dola bilioni 8 kupambana na COVID-19


Mkutano wa G-20 uliofanyika kupitia teknolojia ya video kupitia mtandao.

Kikundi cha nchi ishirini tajiri duniani (G-20) zinazitaka “nchi zote ulimwenguni, taasisi za kimataifa, na watu binafsi” kuchungia juhudi za mfuko wa kupambana na COVID-19, na wameweka lengo la kukusanya dola za Marekani bilioni 8.

Jukwaa la kimataifa linalozileta pamoja serikali na magavana wa mabenki kutoka nchi 19 na Umoja wa Ulaya, nchi za G-20 zimekwisha kusanya dola bilioni 1.9 hadi Ijumaa kwa taarifa yao. Saudi Arabia, ambayo inashikilia hivi sasa urais wa G-20, imechangia dola milioni 500.

“Changamoto za kimataifa zinahitaji suluhisho la kimataifa, na huu ni wakati wetu wa kusimama pamoja na kusaidia mbio hizi za kutafuka chanjo na hatua za matibabu mengine kukabiliana na COVID-19,” Sherpa Fahad Almubarak anayeiwakilisha Saudi Arabia amesema.

“Tunapongeza juhudi zilizopo za kuchangisha fedha kutoka ulimwenguni kote na tunasisitiza umuhimu wa kuziba pengo hili la upungufu wa fedha.”

Uingereza inasema imefanya jaribio la kwanza la chanjo dhidi ya virusi vya corona kwa mwanadamu huko Ulaya.

Watu wawili waliojitolea walipatiwa chanjo hiyo Alhamisi mjini Oxford ambapo timu ya Chuo kikuu hicho ilitengeneza chanjo hiyo katika kipindi chini ya miezi mitatu. Mamia ya watu wengine waliojitolea watapatiwa chanjo kwa ajili ya majaribio, na idadi kama hiyo pia itapatiwa chanjo ya ugonjwa wa uti wa mgongo ili kuweza kulinganisha matokeo ya chanjo hizo mbili. Waliojitolea hawajua ni chanjo ipi wamepatiwa.

Jaribio la chanjo hiyo inatoa matumaini mapya wakati dawa ya kukinga virusi iliripotiwa haikuweza kupambana na virusi vya corona kwa wagonjwa nchini China. Katika jaribio la hapa na pale, Remdesivir, dawa iliyotengenezwa na taasisi ya Gilead Sciences yenye makazi yake California, haikuonyesha manufaa yoyote kwa wagonjwa wa COVID-19, na ilishindwa kupunguza uwepo wa virusi hivyo katika mfumo wa damu mwilini mwao.

Marekani imefanya jaribio la kwanza la chanjo hiyo mwezi Machi huko Seattle, Washington. Canada, Russia na nchi nyingine pia wanashughulika kutengeneza chanjo, lakini wataalam wanasema hata kama itapatikana inayofaa hivi karibuni, utengenezaji wa chanjo hiyo na usambazaji wake unaweza kuchukua mwaka mmoja au zaidi.

Tafiti mbalimbali pia zinaonyesha dawa ya malaria hydroxychloroquine haiponyi virusi hivyo na pengine, ukweli ulivyo, inahatarisha maisha ya wagongwa wa COVID-19.

Rais Donald Trump ameifagilia dawa hiyo kuwa inaponya “inabadilisha mchezo wote” katika kutibu maradhi hayo. Alhamisi, alikanusha kuwa amebadilisha maoni yake juu ya dawa hiyo.

"Kumekuwa na matokeo mengi mazuri ya dawa hiyo, na pengine mengine sio matuzi, hilo sifahamu. Nimesoma tukio moja tu," Trump alisema katika mkutano wake na waandishi wa habari wa kila siku.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG