Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 02:02

Wakristo duniani washiriki katika ibada ya Ijumaa Kuu kupitia mitandaoni kutokana na janga la corona


Hali ya ibada ya Ijumaa Kuu huko Jerusalem kutokana na amri ya kutosongamana katika eneo lolote ikiwemo maeneo ya ibada kuepusha maambukizi ya virusi vya corona.
Hali ya ibada ya Ijumaa Kuu huko Jerusalem kutokana na amri ya kutosongamana katika eneo lolote ikiwemo maeneo ya ibada kuepusha maambukizi ya virusi vya corona.

Mamilioni ya watu duniani wanashiriki katika ibada ya Ijumaa Kuu, siku ambayo Wakristo wanaamini Yesu alisulubiwa msalabani huko Jerusalem.

Ibada hiyo ya siku hiyo tukufu inafanyika tofauti mwaka huu wakati waumini wengi watalazimika kuangalia ibada hiyo kupitia mitandao mbalimbali ya jamii badala ya kuhudhuria makanisani, wakati dunia ikikabiliana na COVID-19.

Sehemu nyingi duniani watu wako majumbani ikiwa ni mkakati wa kuzuia maambukizi ya janga hilo la virusi vya corona.

Zaidi ya watu 1.6 wameambukizwa ugonjwa huo, kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa virusi vya corona cha Johns Hopkins.

Marekani ambayo inamaambukizi zaidi duniani ikiwa na zaidi ya maambukizi 466,000. Nchi mbili zinazofuatia ni Hispania yenye maambukizi 153,222 na Itali ikiwa na maambukizi 143,626.

Marekani inaongoza kwa idadi kubwa ya watu wenye virusi vya corona ambapo hadi jana ilikuwa na zaidi ya maambukizi 466,000.

Uongozi wa Rais Trump unaendelea kuangaza jinsi ya kuruhusu shughuli za kiuchumi kuanza tena, ambazo zilifungwa kutokana na virusi vya corona. Zaidi ya Wamarekani milioni 16 wameomba wasaidiwe na serikali baada ya kupoteza ajira kutokana na janga hili.

Mawaziri wa fedha kutoka kanda ya nchi za Ulaya 19 Alhamisi amekubali katika mpango wa msaada wa zaidi ya nusu trilioni euros kutolewa kwa makampuni, wafanyakazi na wahudumu wa mifumo ya afya ili kujikimu kutokana na athari za kiuchumi zinazotokana na mlipuko wa virusi vya corona.

Hatua hizo zitaziwezesha nchi za Itali na Uhispania zilizoathiriwa zaidi na ugonjwa huo kuweza kupata msaada huo wa kuweza kujikwamua kwa sharti kwamba fedha hizo zitumike kwa mahitaji ya mifumo yao ya afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani Kristalina Georgieva ameonya kuwa janga la virusi vya corona linaweza kupelekea hivi sasa hali mbaya zaidi ya kudumaa kwa uchumi duniani tangu ilivyotokea mwaka 1930.

Georgieva amesema Alhamisi kuwa serikali mbali mbali tayari zimetoa dola trilioni 8 katika programu mbalimbali ili kuwezesha uchumi kuendelea kufanya kazi, lakini fedha zaidi zitahitajika. Amesema nchi zinazoendelea na masoko yanayokua yataathirika zaidi. Faraja ya uchumi kuanza kuimarika itaanza kuonekana mwaka 2021, ameongeza.

XS
SM
MD
LG