Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:09

Ukraine yaendelea kuzuia mashambulizi huku ikikarabati miundombinu ya umeme


FILE PHOTO: Kikosi chaWazimamoto wakizima moto katika kituo cha umeme, wakati Russia ikiendelea na mashambulizi Ukraine huko Zhytomyr, Ukraine, Octoba 18, 2022. State Emergency Service of Ukraine/Handout via REUTERS .
FILE PHOTO: Kikosi chaWazimamoto wakizima moto katika kituo cha umeme, wakati Russia ikiendelea na mashambulizi Ukraine huko Zhytomyr, Ukraine, Octoba 18, 2022. State Emergency Service of Ukraine/Handout via REUTERS .

Majeshi ya Ukraine yamekabiliana na duru mpya ya mashambulizi ya Russia upande wa mashariki, mkuu wa majeshi ya Ukraine alisema.

Wakati huo huo mafundi wanajitahidi kurejesha umeme kufuatia wimbi la mashambulizi ya karibuni ya makombora ya Moscow yaliyosababisha kukatika umeme nchi nzima huku viwango vya joto vikiwa vimeshuka.

Majeshi ya Russia yameendelea na mashambulizi yao bila ya kusita katika maeneo ya Bakhmut na Avdiyivka katika mkoa wa Donetsk, Mkuu wa Majeshi alisema Desemba 6, akiongezea kwamba vifaru na makombora yalishambulia makazi 20 katika eneo hilo, ikiwemo Soledar, Verkhnokamyanske, Andriyivka na Yakovlyivka.

Maafisa wa Ukraine wameonya kwamba miundombinu muhimu ya umeme inaendelea kutishiwa kutokana na mashambulizi zaidi ya Russia na kutakuwa na hali ya kiza cha dharura mara nyingine katika mikoa kadhaa wakati wahandisi wakijitahidi kutengeneza uharibifu huo uliotokana na mashambulizi ya makombora siku moja kabla yaliyoharibu makazi ya watu na kukata umeme.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alitangaza katika hotuba yake ya usiku kuwa watu wanne waliuawa katika mashambulizi ya Russia. Lakini “watu wetu hawatachoka,” alisema jioni ya Desemba 5.

Takriban nusu ya mkoa huo unaouzunguka mji mkuu wa Ukraine utakuwa hauna umeme kwa siku kadhaa zijazo baada ya mashambulizi ya makombora ya Russia kupiga mitambo ya umeme, gavana wa mkoa wa Kyiv alisema.

Mashambulizi ya Desemba 5, ambayo yalizitumbukiza tena sehemu za Ukraine katika kiza chenye baridi kali, yalikuwa ndiyo matokeo ya karibuni katika wiki kadhaa ambayo yamepiga miundombinu muhimu ya nishati.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya Reuters na AFP.

XS
SM
MD
LG