Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 15:12

Serikali ya DRC yamuita balozi wa Rwanda ikidai Kigali inaunga mkono waasi wa M23


Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame, 24 mars 2022, (Présidence Rwanda)
Rais wa DRC Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame, 24 mars 2022, (Présidence Rwanda)

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imemuita balozi wa Rwanda  and kusimamisha safari za Rwandair kwenda Congo ikiwa ni majibu kwa kile ambacho inasema uungaji mkono wa Kigali kwa waasi wa M23 wanaofanya mashambulizi ya kijeshi mashariki mwa Congo.

Rwanda imekanusha kuwasaidia waasi, ambao wamekaribia kiasi cha kilometa 20 wiki hii huko mashariki mwa Congo kuelekea mji wa Goma, na kwa muda mfupi walikamata kambi kubwa ya kijeshi katika eneo hilo.

Wachunguzi wa Congo na Umoja wa Mataifa pia wameishutumu Kigali kwa kuinga mkono M23 wakati wa uasi wa mwaka 2012 – 2013 ambapo kwa muda mfupi waliuteka mji wa Goma. Rwanda ilikanusha madai hayo.

Msemaji wa serikali ya Congo, Patrick Muyaya, alitangaza kusimamishwa kwa safari za shirika la ndege la taifa la Rwanda na kumuita balozi wake Ijumaa usiku, kufuatia mkutano wa baraza la taifa la ulinzi.

Alisema pia mamlaka nchini Congo imelitaja kundi la M23 ni la kigaidi na huenda likaliondoa katika mashauriano ambayo yamekuwa yakifanyika na kusimama katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, kati ya serikali ya Congo makundi yanayofanya harakati zake upande wa mashariki mwa nchi.

“Onyo lilitolewa kwa Wanyarwanda, ambao walikuwa na tabia ambayo huenda ikavuruga mchakato wa amani ambao unakaribi kufikia mwisho katika majadiliano yanayofanyika Nairobi, ambako makundi yote yenye silaha, isipokuwa M23, wana nia ya dhati kuchukua njia ya amani,” alisema Muyaya.

Serikali ya Rwanda haijaweza kupatikana kutoa maoni yake siku ya Jumamosi.

Mapigano katika muda wa zaidi ya wiki moja yamewalazimisha takriban watu 72,00 kukimbia makazi yao, Umoja wa Mataifa ulisema Ijumaa, na kufanya kuwa moja ya hali mbaya ya ukosefu wa makazi barani Afrika.

Mashariki mwa Congo imeshuhudia mizozo ya mara kwa mara tangu mwaka 1996, wakati Rwanda na mataifa mengine jirani yalipoivamia nchi hiyo kuwasaka wanamgambo wa Kihutu ambao walishiriki katika mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994.

XS
SM
MD
LG