Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 17:13

UN yalaani mashambulizi ya waasi wa M23 dhidi ya vikosi vyake DRC


Umoja wa Mataifa umeshutumu mashambulizi dhidi ya kambi zake za kijeshi yaliyofanywa na kundi la waasi wa M23 na kulitaka kundi hilo kuacha mapigano mara moja.

Taarifa iliyoandikwa na umoja huo kwenye ukurasa wa twitter imesifu juhudi zilizochukuliwa na wanajeshi wake kujibu mashambulizi ya waasi hao.

Waasi wa M23 wanawashutumu wanajeshi wa Umoja wa mMataifa kwa kushirikiana na wanajeshi wa serikali pamoja na makundi ya waasi, kushambulia ngome zake.

Mapigano makali yameendelea tangu jumapili, katika eneo la Rutshuru, Kivu kaskazini, na kupelekea maelfu ya watu kukimbilia Uganda kama wakimbizi.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wana ruhusa ya kutumia nguvu kupigana na waasi, lakini raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wanasema kwamba wanajeshi hao hawajafanya vya kutosha kusambaratisha makundi ya waasi yanayo washambulia kila siku.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamekuwa DRC kwa zaidi ya miaka 20.
Mapigano yanaendelea huku serikali ikifanya mazungumzo na makundi ya waasi, namna ya kumaliza vita hivyo.

Mazungumzo yalifanyika Nairobi mwezi uliopita, ambapo waakilishi wa kundi la M23 walifukuzwa kwenye mkutano huo baada ya kushutumiwa kwa kukataa kuacha mapigano.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG