Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 01, 2023 Local time: 18:28

DRC: Waasi wa M23 washambulia kambi za jeshi la serikali


Waasi wa M23 wanaopigana na wanajeshi wa serikali ya DRC

Waasi wa M23 wanakaribia kuteka kambi kumbwa ya wanajeshi mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, baada ya siku kadhaa za mapigano.

Afisa wa jeshi ameambia shirika la habari la AFP kwamba mapigano makali yameendelea katika kambi ya jeshi ya Rumangabo, Rutshuru, kivu kaskaizni, kilomita 40 kutoka mjini Goma.

Msemaji wa jeshi la DRC Generali Sylvain Ekenge, amesema kwamba mapigano yanaendelea tangu asubuhi.

Wakaazi wa Rumangabo wameripoti kusikia milio ya risasi siku nzima, jeshi la DRC likipigana kudhibithi kambi ya Rumangabo.

Jeshi la DRC vile vile limethibitisha kwamba waasi wa M23 wameshambulia kambi za jeshi la serikali za Nyragongo na Rutshuru.

Kulingana na taarifa ya jeshi la DRC, waasi wa M23 wamefyatua zaidi ya roketi 20 katika sehemu za Rumangabo, Natale na sehemu zilizo karibu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG