Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:48

Rais mpya Samia awataka Watanzania waungane


Samia Suluhu Hassan akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na Global Publisher TV, Tanzania.)
Samia Suluhu Hassan akiapa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha na Global Publisher TV, Tanzania.)

Rais mpya wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema hivi leo kuwa nchi ni vyema iungane pamoja na kuepuka kunyoosheana vidole baada ya kifo cha John Magufuli, na kulisihi taifa hilo la Afrika Mashariki kuangalia mbele kwa matumaini na imani. 

Mara baada ya kula kiapo cha kushika rasmi madaraka ya rais, katika sherehe zilizofanyika Ikulu mjini Dar es Salaam, Samia Suluhu amekuwa rais wa kwanza mwanamke katika taifa lenye zaidi ya watu milioni 58.

Samia Suluhu alikuwa makamu rais wa Tanzania tangu mwaka 2015, katika hotuba yake baada ya kuapishwa alisema “wakati umefika wa kuondoa tofauti zetu, na kuwa wamoja kama taifa,” akiongezea kuwa “huu si wakati wa kunyoosheana vidole, lakini ni wakati wa kushikana mikono na kusonga mbele pamoja.”

President Samia akikagua gwaride la heshima baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Photo by Global Publishers TV, Tanzania.
President Samia akikagua gwaride la heshima baada ya kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Photo by Global Publishers TV, Tanzania.

Matamshi yale yalionekana kulenga kuzima hali ya kutokuwa na uhakika ambayo ilijitokeza baada ya Magufuli kukosolewa na upinzani kama mtu ambaye alikuwa na utawala wa kiimla.

Miongoni mwa majukumu ya kwanza ya Samia Suluhu mwenye umri wa miaka 61 ni kufanya maamuzi kama taifa hilo litapokea chanjo ya Covid-19 au la. Chini ya utawala wa kiongozi aliyemtangulia, serikali ilisema haitapokea chanjo ya aina yoyote mpaka watalaamu wa nchi hiyo wazifanyie tathmini tena.

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus alitweet kumpongeza Samia Suluhu na kusema anatazamia kufanya kazi naye na kuwaweka watu wake salama kutokana na Covid 19. Tanzania iliacha kuripoti takwimu za virusi vya corona Mei mwaka jana, jambo ambalo halikufarahiwa na WHO.

Samia Suluhu pia atakuwa na jukumu la kuiponya nchi yake kwa kile ambacho imepitia wakati wa enzi ya Magufuli, wachambuzi wamesema. Huenda akakabiliwa na changamoto ya kujenga wigo wa kisaisa kutawala, kushindana makundi ndani ya chama chake tawala wanaotaka kuonekana baada ya Magufuli kukamata hatamu za uongozi kumzunguka, wachambuzi wanasema, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Rais mpya akielezewa ni mwenye sauti ya upole anaelezewa kuwa uongozi wake huenda ukawa tofauti na wa Magufuli, ambaye alikuwa akipenda umaarufu na kufanya maamuzi yah apo kwa hapo na kujipatia jina la ‘Bulldozer’ na pia kuelezewa ni mtu aliyekuwa hastahmili kukosolewa, jambo ambalo serikali yake ililikanusha.

Alimpongeza marehemu rais katika matamshi yake, na kumuelezea kuwa ni mtu aliyemfundisha mengi, lakini pia aliushukuru upinzani kwa salaam za kumuombea ‘nguvu, faraja na mshikamano’ baada ya kifo cha Magufuli.

XS
SM
MD
LG