Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 22, 2024 Local time: 12:29

Majaliwa akanusha uvumi kuwa Rais Magufuli mgonjwa


Prime Minister Kassim Majaliwa (Courtesy Photo Michuzi Blog)
Prime Minister Kassim Majaliwa (Courtesy Photo Michuzi Blog)

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekanusha habari zilizoenea kwa karibu wiki nzima sasa kwamba Rais John Magufuli ni mgonjwa, akisema kuwa rais “ni mzima na anaendelea na kazi zake kama kawaida”.

Majaliwa ambaye alikuwa akizungumza wakati wa sala ya Ijumaa mjini Njombe, kusini mwa Tanzania aliwataka Watanzania kupuuza ripoti zinazosambaa ambazo zinaeleza kuwa kiongozi wao ni mgonjwa.

Waziri Mkuu, hata hivyo, hakutoa maelezo zaidi kuhusu mahali aliko rais ambaye hajaonekana hadharani kwa takriban wiki mbili sasa huku kukiwa na uvumi kuwa ni mgonjwa sana.

Matamshi ya Majaliwa ni maelezo ya kwanza rasmi kutolewa na serikali ya Tanzania kuhusu kutoonekana hadharani kwa Rais Magufuli na uvumi kuenea kwamba ni mgonjwa mahututi na pengine yuko nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Majaliwa alikuwa mkoani Njombe kusini mwa Tanzania ambako alihudhuria sala ya Ijumaa pamoja na waumini wengine wa kiislamu, amesema kuwa amezungumza kwa simu na Rais.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:19 0:00


Rais Magufuli mwenye umri wa miaka 61, ambaye amepewa jina la utani ‘Bulldozer’ mara ya mwisho alionekana hadharani Februari 27, alipomuapisha Waziri Kiongozi, Dr. Bashiru Ally huko Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Vyombo mbali mbali vya habari vya kimataifa vimekuwa vikizungumzia kuhusu kuugua kwa rais na kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi, lakini msemaji wa Ikulu, Gerson Msigwa pamoja na msemaji wa serikali ya Tanzania, Dkt Hassan Abbas hawajatoa kauli yoyote kuthibitisha au kukanusha ripoti hizo.

Kumekuwepo na ripoti kwamba huenda Rais Magufuli anaugua Covid 19 na hivyo kutokana na matatizo ya moyo aliyonayo huenda alihitajika kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi.

Ripoti hizi zinajitokeza wakati Rais amekuwa mstari wa mbele katika kupuuza kuwa hakuna tishio la Covid 19 nchini Tanzania na kubeza taharuki ambayo imejitokeza kote duniani. Amewasihi watanzania kuweka imani yao katika sala na tiba mbadala za dawa za miti shamba kama vile kujifukiza badala ya chanjo, ambazo amesema ni hatari sana na ni sehemu ya njama za magharibi.

Katika hotuba yake Ijumaa Waziri Mkuu Majaliwa pia aliwanyooshea kidole watanzania ambao wanaishi nje ya nchi kuwa ndiyo vinara wa kueneza habari ambazo si za kweli kuhusu afya ya rais wa Tanzania.

please wait

No media source currently available

0:00 0:00:16 0:00


Itakumbukwa kuwa Tanzania wakati janga la Covid 19 lilipoingia nchini humo Machi mwaka jana, serikali ilikuwa ikitoa takwimu za maambukizi ya virusi vya corona na watu ambao wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo. Mara ya mwisho kutoa ripoti kuhusu janga hilo ilikuwa mwezi Mei ambapo iliripotiwa kuwa kulikuwa na kesi 509 za maambukizi na vifo 21, kwa mujibu wa data za Shirika la Afya Duniani (WHO).

Wakati janga la Covid likiwa linasambaa kote barani Afrika na kuathiri mataifa mengi na hivyo tahadhari na masharti maalum kuchukulia katika juhudi za kuzuia na kujikinga na virusi vya corona, watanzania wao hawakukumbwa na kanuni zozote za kujikinga na hivyo waliruhusiwa kukusanyika pamoja, kwa mfano kwenda kwenye viwanja vya michezo. Rais Magufuli pia alibeza vifaa vya kupima virusi ambavyo viliagizwa kutoka nje, akisema vifaa hivyo pia vilibainisha kuwa mbuzi na mapapai pia yalikuwa yamepata maambukizi ya virusi vya corona.

Lakini katika miezi ya karibuni wasi wasi umeongezeka kuwa Tanzania imekumbwa na janga la Covid hasa baada ya makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad, kufariki kwa Covid 19 mwezi Februari, na chama cha ACT-Wazalendo kutangaza kuwa alikuwa ana maambukizi ya virusi vya corona.

XS
SM
MD
LG