Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 11:43

Magufuli atahadharisha matumizi ya chanjo


Rais John Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amewatahadharisha Watanzania na mataifa mengine ya Afrika juu ya matumizi ya chanjo za magonjwa mbalimbali zinazotoka mataifa nje ya Afrika kwa minajili ya kukabili maambukizi ya magonjwa hayo.

Rais Magufuli akiwa katika hafla ya kitaifa iliyofanyika Chato mkoani Geita Jumatano amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kiafya dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Pia ametoa angalizo kwa watanzania kuacha kukimbilia chanjo dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19 na magonjwa mengine sugu.

Rais Magufuli ingawa hakusema moja kwa moja kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Corona yapo nchini, ametaka tahadhari ichukuliwe ikiwemo wananchi kujifukiza, kula vizuri na pia kuendelea kumuomba Mungu

Rais amewataka watanzania kuendelea kuchapa kazi huku wakichukua tahadhari za kiafya kwa vile hana mpango wa kuzuia watu kutoka nje kwa kusisitiza kuwa taifa la Tanzania halitaweza kujifungia ndani kutokana na changamoto za Corona.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG