Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:39

Raia wa Kenya wapiga kura kwa amani 


Mwananchi wa Kenya akipiga kura katika uchaguzi mkuu Kenya 2022.
Mwananchi wa Kenya akipiga kura katika uchaguzi mkuu Kenya 2022.

Upigaji kura ulikuwa ukiendelea siku ya Jumanne katika uchaguzi usio wa kawaida wa urais nchini Kenya.

Kiongozi wa muda mrefu wa upinzani Raila Odinga ambaye anaungwa mkono na rais anayemaliza muda wake, Uhuru Kenyatta anakabiliana na naibu rais shupavu William Ruto ambaye amejiweka kama mtu asiye kwenye utawala na mtafutaji.

Uchaguzi huo unachukuliwa kuwa na ushindani mkali na kitovu hicho cha uchumi cha Afrika Mashariki ambacho kinaweza kushuhudia duru ya pili ya upigaji kura wa urais kwa mara ya kwanza.

Masuala ya kiuchumi kama vile ufisadi uliyoenea yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko mivutano ya kikabila ambayo imevutia katika upigaji kura wa nyuma na wakati mwingine kupelekea matokeo mabaya.

Kenya ni kinara kwa mfumo wake wa kidemokrasia katika eneo ambalo baadhi ya viongozi wanajulikana kwa kung'ang'ania mamlaka kwa miongo kadhaa.

Utulivu wake ni muhimu kwa wawekezaji wa kigeni, wafanyabiashara wanyenyekevu zaidi wa mitaani na majirani wenye matatizo kama Ethiopia na Somalia.

XS
SM
MD
LG