Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 09:29

Maafisa wa tume ya uchaguzi wakamatwa baada ya kupatikana katika mikutano ya siri


Maafisa wa tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC katika chumba chenye vifaa vya kupigia kura. Aug 7 2017. Picha: Reuters

Maafisa 8 wa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC wamekamatwa na polisi na kusimamishwa kazi baada ya kupatikana katika mkutano wa siri na baadhi ya wagombea wa nafasi tofauti katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Maafisa hao wamekamatwa katika kaunti za Homabay, Kisumu na Bungoma.

Maafisa wengine wanne wa tume hiyo ya uchaguzi wamesimamishwa kazi katika maeneo bunge ya Ndiwa na Webuye mashariki.

Walikuwa wamekutana kwa siri na wagombea wa kiti cha wawakilishi wa bunge la kaunti, na wagombea wa ubunge.

Kukamatwa kwao kulifuatia taarifa za wananchi, ambao waliwapeleka kwa polisi.

Ushahidi wa video uliotolewa kwa polisi, unaonyesha kwamba katika mojawapo ya tukio, naibu wa msimamizi wa kituo cha kupigia kura alikuwa akimshawishi mkubwa wake kukubali “kumsaidia mmoja wa wagombea kupata ushindi.”

Baadhi ya maafisa wengine wa tume ya uchaguzi katika kaunti ya Bungoma wametoroka baada ya wenzao kukamatwa nyumbani kwa mmoja wa wagombea. Mshukiwa aliyekamatwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Webuye.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG