Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 30, 2022 Local time: 22:55

Pompeo : Washington haitakubali Russia kuingilia kati uchaguzi 2020


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, kushoto, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov kabla ya kuanza mazungumzo yao katika Hoteli ya ufukweni iliyoko Bahari Nyeusi, Sochi, kusini mwa Russia, May 14, 2019.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amemwambia Waziri Mkuu wa Russia Sergei Lavrov kwamba utawala wa Washington hautakubali Moscow kuingilia kati uchaguzi mkuu ujao 2020.

Ameeleza kuwa kitendo cha kuingilia uchaguzi mkuu kitaharibu kabisa uhusiano kati ya nchi hizo mbili ambao tayari unayumba.

Katika ziara yake ya kwanza nchini Russia kama Waziri wa Mambo ya Nje, Pompeo alitofautiana hadharani na Lavrov juu ya suala la Ukraine na Venezuela.

Baada ya mkutano huo, Pompeo na Lavrov wamesema hawakukubaliana kuhusu mambo mengi.

Mawaziri hao wameeleza ishara ya kupiga hatua katika kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Russia.

Lakini hawakuthibitisha iwapo Rais Donald Trump atakutana na Vladimir Putin wa Russia, wakati wa kikao cha viongozi wa nchi 20 tajiri zaidi duniani, utakaofanyika Japan, mwezi Juni.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG