Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 20:32

Cohen adai Trump alijua hujuma ya WikiLeaks


Michael Cohen2019.

Wakili wa zamani kwa muda mrefu wa Rais wa Marekani Donald Trump, Michael Cohen, ameliambia jopo la wabunge linalofanya uchunguzi Jumatano kuwa Trump ni "mbaguzi... tapeli na mdanganyifu."

Cohen, wakati anasubiriwa kuanza kuhojiwa, aliwaambia wabunge kuwa Trump alikuwa anajua kuwa mshauri wake wa kampeni Roger Stone alikuwa anafanya mawasiliano na muasisi wa WikiLeaks Julian Assange juu ya kusambazwa kwa barua pepe za Kamati ya Taifa ya Chama cha Demokrat zilizokuwa zimedukuliwa na kutumiwa kumvurugia uchaguzi hasimu wake Hillary Clinton kabla ya kuwekwa katika mitandao kwa ajili ya umma.

Cohen pia anasema Trump alikuwa anajua hilo na alimuelekeza yeye alidanganye Bunge juu ya mazungumzo yaliyofanywa na kampuni ya Trump wakati wa kampeni 2016 juu ya ujenzi wa jengo refu ghorofa huko Moscow, wakati huo akiwa mgombea Trump aliwaambia wapiga kura kuwa alikuwa hana mafungamano yeyote ya kibiashara na Russia..

Cohen amesema Trump alikuwa hajatarajia kabisa kuwa atashinda urais.

"Donald Trump ni mtu ambaye aligombea kuchukuwa madaraka ya uongozi kulifanya jina lake la biashara liwe bora, na siyo kuifanya nchi kuwa bora," Cohen amesema.

"Alikuwa hana nia au utashi wa kuliongoza taifa -- bali kujitangaza yeye mwenyewe na kujenga utajiri wake na kujipatia madaraka. Kampeni -- yake -- ilikuwa siku zote ni fursa ya kutangaza biashara yake."

Cohen, alieleza uzoefu wake katika kumfanyia kazi zake Trump kuwa ilikuwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10, "Ni mbaguzi. Ni tapeli. Na ni mdangayifu."

Ushahidi anaotoa Cohen unakuja takriban miezi miwili kabla ya kuingia jela kwa kifungo cha miaka mitatu baada ya kukiri kujihusisha na jinai za kifedha, kukiuka utaratibu wa utoaji fedha katika kampeni unaofungamana na uchaguzi wa 2016 na kulidanganya Bunge.

Trump, akiwa Vietnam kuhudhuria mkutano kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jung Un, alimshambulia wakili wake wa zamani kupitia ujumbe wa Twitter kabla ya kuanza kutoa ushahidi, akisema "alikuwa punde to amezuiliwa na Mahakama ya Juu kwa sababu ya kudanganya na wizi. Alikuwa amefanya mambo maovu yasiyohusiana na Trump. Anasema uongo ili apunguziwe muda wake wa kukaa jela.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG