Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 05:49

New Zealand yaruhusu shule, biashara kufunguliwa baada ya kudhibiti COVID-19


Waziri Mkuu Jacinda Ardern

New Zealand imeingia katika hatua mpya katika amri kali iliyokuwa imeiweka wakati huu wa janga la virusi vya corona Jumatatu ambapo baadhi ya shule na biashara zimefunguliwa tena.

Serikali imeripoti leo maambukizi matano mapya tu na Waziri Mkuu Jacinda Ardern amesema mamlaka husika zitaendelea kufuatilia maambukizi yoyote yale mapya. New Zealand inamaambukizi 1,100 yaliyothibitishwa kwa vipimo na vifo 19.

“Hakuna maambukizi yalioenea, na kushindwa kutambuliwa katika jamii nchini New Zealand,” Ardern ametangaza. “Tumeshinda vita hiyo.”

Kulegezwa kwa masharti hayo kutaruhusu watu 400,000 kurejea makazini.

Ni kipindi cha mwezi mmoja tangu New Zealand ilipowataka watu kutotoka majumbani na kuamuru shughuli zote ambazo siyo muhimu kufungwa.

Ardern amesema ni mapema mno kusema lini nchi hiyo itafikia kuwa haina maambukizi ya COVID-19, hatua ambayo ni muhimu kuweza kufunguwa tena kikamilifu shughuli zote nchini.

Mkakati wa Australia

Sehemu ya mkakati wa kufungua tena shughuli kama kawaida katika nchi jirani ya Australia ni kupitia matumizi ya simu za kisasa zenye app ambayo kusudio lake ni kusaidia serikali za majimbo na wafanyakazi wa afya kufuatilia mawasiliano ya karibu na watu wengine ya wale ambao wamepimwa na kuthibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Ufuatiliaji huo unasaidia mamlaka husika kufahamu nani anatakiwa ajitenge yeye mwenyewe na nani atahitaji kuchukuliwa vipimo ili kuzuia kueneza ugonjwa huo.

Waziri wa Afya Greg Hunt amesema Jumatatu mchana takriban wananchi wa Australia milioni 2 walikuwa wamepakua app hiyo katika simu zao za kisasa.

Baadhi ya nchi zilizokuwa zimeathirika zaidi na janga hilo zimeripoti kupungua kwa idadi ya vifo vya kila siku Jumapili, ambapo Itali, Uhispania na Uingereza zimesema kiwango cha vifo kimeshuka chini kabisa kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Uingereza

Uingereza ilimkaribisha Waziri Mkuu Boris Johnson kazini Jumatatu baada ya kuwa kiongozi wa kwanza wa dunia kuambukizwa COVID-19 na kuwekwa siku kadhaa katika wadi ya wagonjwa mahtuti.

Alizungumza nje ya Ofisi ya Downing Street, akisema kuwa wakati anafahamu watu hawana uvumilivu tena na wana wasiwasi, kulegeza masharti hivi sasa itahatarisha “wimbi jipya la vifo na ugonjwa huo” litakalo athiri zaidi uchumi.

“Sitaki kupoteza juhudi yote na kujitolea kote kuliko fanywa na watu wa Uingereza na kuhatarisha kuwepo kwa mlipuko mwengine mkubwa na hasara kubwa ya watu kufa na Mifumo ya Afya ya Taifa kuelemewa,” amesema.

“Nataka mudhibiti hamasa zenu, kwa sababu naamini hivi sasa tunakaribia kufikia mwisho wa awamu ya kwanza ya janga hili. Na japokuwa tumekabiliwa na matezo yote haya, lakini tunakaribia kufikia mafanikio.

Wakati huo huo Itali inatizamia kulegeza masharti ya kutotoka nje kuanzia wiki ijayo.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte amesema watu wataruhusiwa kutembelea ndugu zao katika makundi madogo, lakini itawalazimu wavae maski usoni. Viwanja vya umma vimepangwa kufunguliwa, lakini shule zitaendelea kufungwa hadi September.

Conte amesema hakuna maamuzi yaliyofikiwa lini ligi ya soka ya kundi A, lakini mchezaji mmoja mmoja anaweza kuanza mazoezi Mei 4 na timu zinaweza kukusanyika kwa ajili ya matayarisho Mei 18. COVID-19 imeuwa takriban watu 27,000 nchini Itali.

Mlipuko wa corona umepelekea ligi za soka kufungwa duniani kote, na njia moja ambayo wanariadha na washabiki wanakabiliana na hilo ni kucheza game za video.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG