Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:20

Kiongozi wa mrengo mkali wa kulia Bennett adhamiria kumuondoa Netanyahu madarakani


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Wananchi wa Israeli wamegawika kufuatia habari kwamba kiongozi wa chama cha mrengo mkali wa kulia Naftali Bennett atajiunga na serikali ya umoja wa kitaifa kwa lengo la kumondoa madarakani Waziri Mkuu wa muda mrefu Benjamin Netanyahu.

Wachambuzi wa kisiasa nchini humo wanasema hatua hiyo huenda ikawa ndio mwisho wa enzi ya kisiasa na kiongozi huyo wa mrengo wa kulia anaekabiliwa na mashtaka ya ulaji rushwa.

Uamuzi wa Naftali Bennet kutangaza Jumapili katika hotuba kwa taifa huenda sasa ukamwezesha kiongozi mkuu wa upinzani Yair Lapid kuunda serikali ya mseto itakayounganisha pamoja vyama vya mrengo wa kulia, kati na kushoto vya israeli na kumshinda kwa mara ya Kwanza Netanyahu tangu mwaka 1996 alipochukua uongozi wa serikali nchini humo.

Akilihutubia taifa hapo jana mwanasiasa mwenye siasa kali za kizalendo za mrengo wa kulia, kiongozi wa chama cha Yamina Bennett alisema yuko tayari kujiunga na mungano huo ambao vyombo vya habari vya Israel vinautaja ni muungano wa mageuzi.

Bennett mkuu wa chama cha Yamina ameeleza kuwa : "Vyama vyote vimealikwa kujiunga na serikali. Kwa serikali itakayofanikiwa, ambapo vyama vyote vitahitajika kuwa na ustahamilivu wakati wa majadilianio na hata baadae. Hakuna mtu anaeombwa kuacha kando itikadi zake lakini kila mmoja anatakiwa kuweka kando malengo na ndoto zao kwa sasa.

Wabunge wote wanaompinga Netanyahu wamekuwa katika majadiliano magumu kabla ya Jumatano siku ya mwisho kwa Lapid, mwenye umnri wa miaka 57 anaye kiongoza chama cha mrengo wa kati, Yesh Atid, kutangaza serikali yake wakati makubaliano ya kusitisha mapigano na Hamas yakiheshimiwa.

Na kufuatana na makubaliano yaliyofikiwa kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Israeli ni kwamba Bennet atachukua nafasi ya Netanyahu kama Waziri Mkuu na baadae kumkabidhi Lapid chini ya makubaliano ya Kubadilishana uongozi.

Netanyahu anaekabiliwa na mashtaka ya uhalifu kwa ajili ya ulaji rushwa na kuchukua hongo aliyeshikilia madaraka katika kipindi cha msukosuko wa kisiasa ambapo hakuweza kuunda serikali baada ya kufanyika uchaguzi mara nne katika kipindi cha mwaka moja alilihutubia taifa na kusema serikali hiyo mpya itakuwa ni hatari kwa usalama wa taifa.

Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel ameeleza : "Hivi sasa tuko katika wakati nyeti kwa ajili ya usalama, umbo na mustakbali wa taifa la Israeli. Katika wakati muhimu kama huu mtu anabidi kuweka kando maslahi yake binafsi na kuchukua hatua za kipekee. Ndio maana ninatoa wito kwa wafuasi wote wamrengo wa kulia kuungana kuzuia kuundwa kwa setikali ya mrengo wa kushoto.

Mvutano huo wa kisiasa unamulika jinisi Waisrael wenyewe walivyogawika. Elisheva Libeler mkazi wa Jerusalem anasema si haki namna mambo yanavyo kwenda.

Elisheva Libeler, mkazi wa Jerusalem ameeleza : "Ninadhani ni jambo la aibu kwa mtu aliyepata viti 7 pekee yake kuamua hatma ya nchi. Kulikuwa na wengi wa wapiga kura waliomchagua mtu mmoja na ikiwa haiwezekani inabidi uchaguzi mpya ufanyike.

Libeler anachukulia kwamba chama cha Likud cha Netanyahu kilipata viti vingi na vipi Bennett mwenye viti sita katika Bunge la viti 120 anakuwa Waziri Mkuu.

Moshe Hain mkazi pia wa Jerusalem akizungumza na shirika la habari la Reuters anasema hali ni tete kabisa na wafuasi wengi wa Bennett wamesikitishwa.

Moshe Hain, mkazi wa Jerusalem ameeleza : "Mimi ninadhani huu ni wakati muhimu kabisa kwa Israel na siasa zake na kwa Bennett mwenyewe. Amechukua hatua ya bahati nasibu. Anaweza kuunda serikali ya mrengo wa kulia kama anavyotaka au atashindwa."

Wachambuzi wanasema itakuwa vigumu kuunda serikali ya mrengo wowote kwani vyama vimeungana kumondoa Netnayahu baada ya miaka 12 madarakani. Lapid anaahidi Jumatano kuunda serikali itakayoungwa mkono na wabunge 61.

XS
SM
MD
LG