Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 06, 2024 Local time: 00:50

Israel na Hamas waanza sitisho la mapigano lisilo na masharti


Rais Joe Biden akizungumzia sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas, huko White House, Alhamisi Mei 20, 2021, in Washington. (AP Photo/Evan Vucci)
Rais Joe Biden akizungumzia sitisho la mapigano kati ya Israel na Hamas, huko White House, Alhamisi Mei 20, 2021, in Washington. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais wa Marekani Joe Biden alisema Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alimjulisha Alhamisi kwamba Israeli imekubali kusitisha mapigano ya pande zote, bila masharti na kundi la wanamgambo la Hamas.

Makubaliano ya sitisho la mapigano lilipangwa kuanza saa 8 usiku saa za huko Ijumaa yatarejesha utulivu kwa Israeli na Gaza.

Hamas imefyatua roketi katika miji ya Israeli kutoka Gaza tangu Mei 10, kwa kile ilichosema ni ukiukwaji wa haki uliofanywa na Israeli dhidi ya Wapalestina huko Jerusalem.

Israeli ilikuwa ikilipiza kisasi kwa makombora ya kulenga na mashambulizi ya anga kwa viongozi wa Hamas na miundombinu ya kundi hilo. Waisraeli walikabiliwa na shutuma ya kimataifa kwa kulipua majengo yenye urefu wa juu na kupiga kambi za wakimbizi na malengo mengine, ambayo yalisababisha vifo vingi vya raia.

Tulifanya mazungumzo mazito ya kiwango cha juu, saa kwa saa, haswa, alisema Biden juu ya kile alichokiita diplomasia ya utulivu ya Marekani kufikia makubaliano.

Rais huyo wa Marekani amesema amezungumza na Netanyahu mara sita katika kipindi cha siku 11 zilizopita kama sehemu ya juhudi za kidiplomasia za utawala wake nyuma ya pazia kufanikisha sitisho la mapigano.

XS
SM
MD
LG