Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 15:36

Juhudi za kuimarisha kusitishwa mapigano kati ya Israeli na Hamas zachukua sura mpya


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu katika mkutano na waandishi wa hatari Mei 25, 2021, Jerusalem, Israel. (AP Photo/Alex Brandon, Pool)
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken akiwa na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu katika mkutano na waandishi wa hatari Mei 25, 2021, Jerusalem, Israel. (AP Photo/Alex Brandon, Pool)

Juhudi za kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas, zinaendelea pale wajumbe wa pande zote wanakutana mjini Cairo, Jerusalem na Ramallah Jumapili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Gabi Ashkenazi amekutana na waziri mwenzake wa Misri Sameh Shoukray mjini Cairo.

Pia mkuu wa idara ya ujasusi wa Misri Abbas Kamel amekutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mjini Jerusalem, kuzungumzia juu ya kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na kuimarisha ushirikaino kati ya nchi hizo mbili.

Kemal alikutana pia na Rais Mahamoud Abass mjini Ramallah kwa mazungumzo kama hayo.

Wachambuzi wanasema Wapalestina kwa muda mrefu wamekuwa wamegawika kati ya Hamas na Fatah lakini mapigano ya hivi karibuni kati ya Israel na Hamas yameweza kuunganisha pande hizo mbili za Wapalestina katika njia ambayo haijawahi kushuhudiwa kwa miaka mingi.

XS
SM
MD
LG