Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 13:55

Maisha yarudi kua ya kawaida Gaza baada ya mashambulizi ya Israel


Wakazi wa Gaza wakikusanya baadhi ya mali zao kutoka vifusi vya jengo la Al-Jawhara lililobomolewa na makombora ya Israel
Wakazi wa Gaza wakikusanya baadhi ya mali zao kutoka vifusi vya jengo la Al-Jawhara lililobomolewa na makombora ya Israel

Maelfu ya wakazi wa Ukanda wa Gaza wamekuwa polepole wakiijarbu kurudi katika maisha yao ya kawaida wakiondoa vifusi na uchafu kutokana na uharibifu uliofanywa na makombora ya Israeli.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuanzishwa utaratibu wa dhati wa kisiasa ili kuzuia kutokea tena umwagaji damu baina ya Israeli na Palestina.

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kutokana na upatanishi wa Misri yamerudisha utulivu siku ya Ijumaa baada ya siku 11 ya mashambulio ya makomboro kutoka ndege za kijeshi za Israel katika kujibu mashambulio ya roketi yalitofanywa na wanamgambo wa kislamu wa Hamas na Islamic Jihad.

Ujumbe wa UN ukiongozwa na mkuu wa idara ya wakimbizi wa Palestina, UNRWA Philippe Lazzarini, ulitembelea maeneo ya Gaza mwishoni mwa wiki na kutoa wito wa kutolewa msaada wa kukarabati ukanda huo pamoja na kuanzisha juhudi za dhati za kubuni mazingira mapya ya kisiasa.

Philippe Lazzarini
Philippe Lazzarini

Lazzarini, Mkuu wa idara ya wakimbizi, UNRWA, anaeleza : "Hii ni mara ya pili kwangu mimi kusimama hapa Gaza baada ya mgogoro kama mjumbe wa jumuia ya wafanyakazi wa huduma za dharura na hili linanikera sana. Maisha magumu yaliyopo Gaza yanazidi kuwa mabaya zaidi kwa sababu msingi wa matatizo ya ugomvi huu hayajatanzuliwa badio."

Wajumbe wa UN na wa mashirika mengine ya huduma za dharura wanapotembelea Gaza kutathmini hasara na msaada unaohitajika, tayari msaada wa kwanza wa dharura umewasili kutoka Misri kupitia kituo cha mpakani cha Raffa.

Pia wakazi wenyewe wa Gaza wamekuwa wakitafuta chochote kile kilichobaki ndani ya vifusi na kujitengenezea mahala ya kuishi. Nazmi Al-Dahdouh alyeshuhudia vita vitatu ameamua kujitengenezea hema kuishi akisema amechoshwa na pande zote.

Nazmi Al-Dahdouh Mpalestina aliyebomolewa nyumba yake Gaza anaeleza : "Nitakwenda wapi hivi sasa? Ninaona watu wamebomolewa makazi yao wakenda katika shule za UNRWA na hawapewi chakula wanahisi wamedharauliwa na kuaibishwa. Kwa hivyo nimeamua kujenga hema langu na kuishi hapa hadi hali itakapobadilika.

Halio hiyo inawakumba Wapalestina elfu 6 waliopoteza makazi yao kutokana na mapigano hayo yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 232 kwenye ukanda wa Gaza kulingana na UN.

Sameh Shoukrty waziri wa mambo ya nje wa Misri (kati) wakati wa mkutano na waandishi mjini Ramallah
Sameh Shoukrty waziri wa mambo ya nje wa Misri (kati) wakati wa mkutano na waandishi mjini Ramallah

Wakati Maisha yakirejea kuwa ya kawaida wanadiplomasia wameanza juhudi za kutafuta suluhisho la kudumu, pale Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry alipowasili Ramallah, Ukingo wa Magharibi, kwa mazungumzo na Rais Mahamoud Abbas.

Naye Mfalme wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani alikutana na Mkuu wa Kisiasa wa Hamas Ismaail Haniyeh mjini Doha.

Na kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza ziara muhimu ya Mashariki ya Kati hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG