Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 19:13

Serikali ya Marekani yafanya mazungumzo na washirika wenye ushawishi Mashariki ya Kati


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili katika uwanja wa ndege wa
kijeshi Andrews Air Force Base, Md, May 16, 2021.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi Andrews Air Force Base, Md, May 16, 2021.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amefanya mazungumzo Jumapili na washirika muhimu wenye ushawishi Mashariki ya Kati wakati Marekani inataka kuzuia kusambaa kwa mapigano mabaya kati ya Israeli na Wapalestina.

Blinken, ambaye alikuwa safarini Jumapili kwenda Denmark mwanzoni mwa wiki ya kidiplomasia ikilenga Arctic, alizungumza kwa simu na maafisa wa Qatar, Saudi Arabia, Misri na Ufaransa.

Baada ya Iran, Qatar inaonekana kuwa na ushawishi mkubwa kwa kundi la wanamgambo wa Hamas.

Waziri huyo alisisitiza wito wake kwa pande zote kuacha mivutano na kusitisha mapigano, ambayo yamepoteza maisha ya raia wa Israeli na Wapalestina, pamoja na watoto, msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ned Price alisema.

Kila wito wa Blinken ulisikika kutoa ujumbe huo, kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Wito huo ulifuata siku mbaya zaidi katika kipindi cha karibu wiki moja, wakati mashambulizi ya Israeli yaliwaua Wapalestina 42 huko Ukanda wa Gaza na wakati Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likifanya mkutano wao kwa njia ya mtandao kati kati ya tahadhari ya ulimwengu juu ya mzozo huo.

XS
SM
MD
LG