Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:35

Kenya : Mwandishi Wainaina aaga dunia


 Binyavanga Wainaina
Binyavanga Wainaina

Mwandishi na mwanaharakati wa uhusiano wa jinsia moja Binyavanga Wainaina, amefariki akiwa na umri wa miaka 48.

Wainaina ambaye ni raia wa Kenya alipinga unyanyapaaji kwa kutumia uandishi wa mafumbo na kukabiliana na ubaguzi wa kijinsia.

Binyavanga alishinda tuzo ya mwandishi bora ya Caine, mwaka 2002 kutokana na uandishi wake wa hadithi fupi kwa jina discovering home yani kutambua nyumbani, iliyofuatiwa na jarida kwa jina ‘kwani’, iliyopelekea kutambuliwa kwa waandishi wengine kadhaa wa Afrika.

Wainaina alikuwa maarufu kutokana na uandishi wake wenye ucheshi ulipopewa jina la “how to write about Afrika”, yani, jinsi ya kuandika kuhusu Afrika, uliopata umaarufu kote duniani baada ya video ya muigizaji wa Hollywood Djimon Hounsou akisoma kazi yake, kuwekwa kwenye internet.

Mwaka 2014, Wainaina aliangaziwa sana na vyombo vya habari alipotangaza kwamba alikuwa katika uhusiano wa jinsia moja, wakati kulikuwepo mjadala mkali kuhusu haki za mashoga barani Afrika.

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters wakati huo, Wainaina alisema alikuwa na hofu kwamba jamii ilikuwa inaendelea kukosa uvumilivu dhidi ya watu walio katika uhusiano wa jinsia moja, na kuwalazimu kujificha.

Wainaina, aliyeugua kiharusi mwaka 2015, alikuwa ametangaza mipango yake ya kuoa mpenzi wake nchini Afrika kusini, mwaka uliopita 2018.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG