Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 24, 2024 Local time: 22:33

Reginald Mengi, mfanyabiashara mshuhuri Tanzania aaga dunia


Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP Tanzania akutana na wanawake wajasirimali
Reginald Mengi Mwenyekiti wa IPP Tanzania akutana na wanawake wajasirimali

Mwenyekiti wa makampuni ya IPP ya Tanzania, Reginald Mengi amefariki dunia kulingana na kituo cha habari cha ITV .

Reginald Mengi ni mmoja wa wafanyabiashara mahiri wa Tanzania, na ukanda wa Afrika Mashariki, ambaye aliwekeza katika sekta za viwanda, na habari.

Habari ambazo zimethibitishwa na kituo cha habari cha ITV, kilipozungumza na VOA asubuhi ya leo, inaelezwa Mengi amefariki dunia usiku wa leo, licha ya kutotoa taarifa zaidi.

Chini ya umiliki wake kupitia makampuni ya IPP, Mengi alianzisha kampuni ya vyombo vya habari ya IPP Media, ambayo ina miliki vituo vya habari vya ITV, East Africa TV, Capital TV, Radio One, East Africa Radio, na Capital FM. Vilevile chini ya IPP Media, Mengi alikuwa akimiliki kampuni ya uchapishaji magazeti ya The Guardian Limited, yenye kuchapisha magazeti ya Nipashe, Alasiri, na the Guardian.

Hivi karibuni Reginald Mengi alitangaza kufanya uwekezaji katika kiwanda cha kuunganisha magari pamoja na simu za mikononi.

XS
SM
MD
LG