Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 03, 2022 Local time: 21:30

Mwanamuziki mwanaharakati wa Zimbabwe Oliver Mtukudzi aaga dunia


Oliver Mtukudzi

Mwanamuziki mashuhuri na mkongwe , Oliver Mtukudzi amefariki dunia nchini Zimbabwe.

Kwa mujibu wa mtandao wa NewsDay la Zimbabwe mwanamuziki huyo alifariki Jumanne mchana katika kliniki ya Avenues iliyoko mjini Harare.

Mtukudzi alizaliwa September 22, mwaka 1952. Mwaka jana alilazwa hospitali baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Licha ya kuitangaza Zimbabwe duniani kupitia kwa muziki wake, pia alikuwa ni mpigania haki za binadamu duniani pamoja na kuwa balozi wa hisani wa shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Mpaka kifo chake mtukudzi alitoa Zaidi ya albamu 60.

Safari yake ya muziki ilianzia mwaka 1977, alipojiunga na bendi ya Wheels ambako alikuwa akiimba na Thomas Mapfumo ambako walitoa muziki wao wa kwanza wa Dzandimomotera ambao ulifanya vizuri sana na kupelekea utoaji wa albamu yao ya kwanza ambayo pia ilifanya vizuri katika soko la muziki.

Sauti yake yenye mvuto wa kukwaruza , imekuwa ndio utambulisho mkubwa ndani na nchi ya Zimbabwe. Nyimbo zake nyingi alikuwa akiimba kwa lugha yake ya Shona na kundi lake la Zimbabwe KoreKore . Pia huchanganya na lugha na midundo ya asili na kufanya muziki wake uwe na mvuto wa kipekee.

Wanamuziki wengi wa Zimbabwe na wa Afrika wamenufaika na mafunzo ya kimuziki kwa njia moja ama nyingine katika kipindi chote cha maisha yake ya kimuziki. Mwaka 2010 alituzwa award kutoka chuo kikuu cha Zimbabwe, ambako alipopewa award na The internation Concil of Afrinana Womenism Award katika mchango wake mkubwa wa kuwainua wanawake kupitia Sanaa ya muziki.

Mtukudzi amefariki akiwa na umri wa miaka 66, alikuwa baba wa watoto watano na wajukuu wawili. Alikuwa kati ya watoto sita , wa kike wanne na wa kiume wawili.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Honeymoon Al-jabri, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG