Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 27, 2023 Local time: 04:08

Gwiji wa muziki Aretha Franklin atoka hospitali


Aretha Franklin akitumbuiza April 19, 2017, mjini New York.

Mwanamuziki Aretha Franklin amehamishwa kutoka hospitali baada ya kulazwa siku chache zilizopita.

Malkia huyu wa Soul imeripotiwa alikuwa na hali mbaya sana kitu kilichopelekea wasanii wengi wakubwa wa Marekani kutoa pole na kumuombea apate nafuu.

Aretha Franklin anaripotiwa kutoka hospitalini na kuungana na familia yake akiendelea kupata nafuu huku akipatiwa matibabu akiwa nyumbani .

Mwimbaji gwiji Aretha Franklin, nyota aliyewahi kushinda tuzo mbalimbali za Grammy.

Aretha ambaye athari za muziki wake zinaenda miongo kadhaa nyuma, hali yake ni mahtuti na hivi sasa amezungukwa na wanafamilia, mwandishi mmoja ambaye ni rafiki wa familia yake ameandika hilo katika tovuti yake Jumatatu.

Franklin, Gwiji wa muziki wa Soul aliyejulikana kama “Queen of Soul” maarufu kwa muziki wake unaoitwa “Respect” (1967) na mwengine “I Say a Little Prayer” (1968), yuko taabani huko Detroit.

Familia yake inawaomba watu kumuombea na pia kuwapa fursa ya kuwa na faragha katika kumuuguza mgonjwa,” ameandika Roger Friedman katika tovuti ya Showbiz 411.

Franklin, ambaye aligunduliwa kuwa na saratani mwaka 2010, alitumbuiza Novemba 2017 katika hafla ilioandaliwa na taasisi ya Elton John AIDS Foundation huko New York.Onyesho lake la mwisho lilikuwa Philadelphia Agosti 2017.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG