Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 02:57

Museveni atoa wito hospitali zitumike kutibu wagonjwa wa maradhi ya Ebola


Rais wa Uganda Yoweri Museveni

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, katika hotuba yake kupitia televisheni, amewataka watu wawe watulivu akisisitiza matibabu rasmi yatumike kwa wagonjwa wa Ebola au wenye kushukiwa kuwa na Ebola.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni, katika hotuba yake kupitia televisheni, amewataka watu wawe watulivu akisisitiza matibabu rasmi yatumike kwa wagonjwa wa Ebola au wenye kushukiwa kuwa na Ebola.

Wito wake umekuja wakati virusi hatari vya Ebola vimekuwa vikienea kama ilivyotangazwa mwezi uliopita.

Kwa mara ya pili tangu mlipuko wa Ebola, Rais wa Uganda Yoweri Museveni amelihutubia taifa kuhusu hatua zilizokusudiwa katika kuzuia kuenea zaidi kwa Ebola.

Museveni alisema serikali ya Uganda imeanzisha vituo kadhaa vya matibabu katika “maene oyenye hatari zaidi” ikiwemo wilaya kadhaa ambako ugonjwa huu umethibitishwa. Akiongeza, serikali inaongeza mifumo ya kutambua wanaokutana na wagonjwa ili kuwatibu wale wenye virusi.

Akizungumza kwa lugha zote, Kiluganda, na Kiingereza, alisisitiza haja ya kupata matibabu rasmi wakati watu wanaambukizwa virusi vya Ebola au kushukiwa kuwa navyo.

“Huwezi kuwa katika eneo la mizimu na au katika nyumba ya kaka yako na kufikiria utapata msaada kuliko ule utakaopata ukienda katika hospitali ya serikali… vipi watadhibiti joto la mwili wako… na nani atakuhudumia na kuwa salama. Hawana vifaa watu hawa,” alisema Museveni.

Aliongeza kuwa, “ waganga wa jadi, waasili na mitishamba wasikubali kuwapokea wagonjwa hivi sasa.”

Mwezi uliopita, Uganda ilithibitisha kuwepo mlipuko wa aina mpya ya kirusi cha Ebola cha Sudan.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ilisema kuwa kulikuwa na maambukuzi ya Ebola 54 yaliyothibitishwa na vifo 19 tangu kuanza kwa ugonjwa huu uliporipotiwa awali katika wilaya ya kati ya Mubende, Septemba 20.

Waziri wa Afya wa Uganda, Ruth Jane Aceng, amethibitisha kuwa nchi hiyo imepokea chanjo za virusi vya Ebola iliyotolewa msaada na Marekani na Uingereza.

Baadhi ya taarifa katika repoti hii inatokana na shirika la habari la AFP

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG