Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 05:00

WHO: Mlipuko wa Ebola Uganda ulianza Agosti na sio Septemba


Wafanyakazi wa afya katika hospitali ya Mubende ambapo mlipuko wa Ebola umeripotiwa. Sept 24 2022. Picha: AFP
Wafanyakazi wa afya katika hospitali ya Mubende ambapo mlipuko wa Ebola umeripotiwa. Sept 24 2022. Picha: AFP

Ofisi ya shirika la afya duniani inayoshughulikia mataifa ya Afrika imesema kwamba mlipuko wa virusi vya Ebola unaoendelea Uganda uligunduliwa kwa kuchelewa.

Uchunguzi wa awali unaashiria kwamba mgonjwa wa kwanza wa virusi hivyo huenda alipata dalili za maambukizi hapo mwezi Agosti lakini hakukutambua alikuwa anaugua ebola.

Watu 24 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola aina ya Sudan. Watu wanne wamefariki.

Dalili za virusi vya Ebola aina ya Sudan zinafanana na dalili za maambukizi ya malaria na homa ya tumbo, ambayo ni magonjwa yanayotokea katika mara katika sehemu ambazo ebola umeripotiwa Uganda na hivyo kuwa vigumu kwa madaktari kugundua ebola kwa haraka.

Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan

XS
SM
MD
LG