Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 13:44

Museveni: mlipuko wa Ebola Uganda umedhibitiwa


Katibu wa kudumu katika wizara ya afya ya Uganda Diana Atwine akihutubia waandishi wa habari jijini Kampala. sept 20 2022. Picha: AP
Katibu wa kudumu katika wizara ya afya ya Uganda Diana Atwine akihutubia waandishi wa habari jijini Kampala. sept 20 2022. Picha: AP

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amehakikishia nchi hiyo kwamba mlipuko wa virusi vya Ebola umedhibitiwa na hakuna amri ya kuzuia watu kusafiri au kuzuia shughuli zao za kawaida itatolewa.

Maafisa wa afya nchini Uganda wamethibitisha kwamba watu sita wamefariki na wengine 31 kuambukizwa virusi vya Ebola aina ya Sudan.

Muungano wa madaktari nchini Uganda umesema kwamba baadhi ya wanachama wake wameambukizwa virusi hivyo na madaktari wametishia kuungana na madaktari wanafunzi kutaka kupewa vifaa vya kujikinga wakiwa kazini.

Museveni amehimiza raia wa Uganda kuchukua kila tahadhari kuepuka maambukizi ya Ebola.

Japo chanzo cha mlipuko huo wa virusi vya Ebola vya Sudan hakijagunduliwa, Museveni ameonya watu dhidi ya kula nyama ya tumbili, nyani na sokwe.

Kati ya watu 31 ambao wamethibitihswa kuambukizwa Ebola, sita ni maafisa wa afya.

Hakuna chanjo dhidi ya virusi vya Ebola aina ya Sudan.

Watu 200 walifariki kutokana na mlipuko wa Ebola nchini Uganda, mwaka 2000.

XS
SM
MD
LG