Katika mkutano wa Jumanne huko White House huku kukiwa na uwezekano wa sitisho la mapigano kati ya Hamas na Israel kuvunjika.
Wapalestina humo Ukanda wa Gaza wanahofia kurejea kwa vita baada ya Hamas kutishia kuchelewesha mpango ujao wa kuwaachia mateka wa Israel na wito wa Rais wa Marekani Donald Trumop kufuta sitisho la mapigano.
Samia Jamal, Mkazi wa Gaza anasema: “Tumechoshwa na vita. Tumeanza kuomba vifo.”
Alipokuwa Mfalme Abdulla II wa Jordan huko White House Jumanne, Trump aliongeza maradufu mpango wake wa kuichukua Gaza.
Rais Donald Trump alisema: “Nadhani kitakuwa kitu ambacho ni kizuri sana Wapalestina. Watakipenda sana. NImefanya vizuri sana katika biashara ya majumba. Naweza kukuelezea vizuri kuhusu biashara hii. Watakuwa na mapenzi nacho makubwa.”
Wapalestina, pamoja na Jordan, Misri na nchi kadhaa nyingine, wamepinga mpango wa Trump wa kuwaondoa kwa nguvu na kuwahamaisha takriban wakazi wa Gaza milioni 1.9 kwenda katika nchi Jirani.
Mbali na kusema kuwa haraka atawapokea watoto 2,000 wanaoumwa wa huko Gaza wenye saratani na magonjwa mengine,
Mfalme Abdulla alitakaa kukubaliana na pendekezo la Trump.
Abdullah II, Mfalme wa Jordan anaeleza: “Nadhani tunapaswa kukumbuka kuwa kuna mpango kuotka Misri na nchi za Kiarabu. Tumekaribishwa na Mwana Mfalme wa Saudi Arabi Mohammed bin Salman kufanya majadiliano huko Riyadh. Nadhani suala lililopo ni jinsi gani tunafanya kazi hii kwa nia ambayo ni nzuri kwa kila mtu.”
Ni mkutano wa hali ya juu kwa Abdulla, ambaye lazima adumishe uhusiano na mshirika mkuu ambaye Jordana anamtegemea wa misaada ya kigeni.
Trump alidokeza Jumatatu kuwa atazuia misaada lakini Jumanne hakufanya hivyo.
Raia wengi wa Jordan ni wa asili ya Wapalestina waliokoseshwa makazi. Kama Abdullah akiunga mkono mpango wa Trump, itasababisha matatizo makubwa ya kisiasa na kiuchumi kwa kuwaruhusu Hamas kuingia, anasema Ghaith al-Omari wa Taasisi ya Washington kwa sera za Mashariki ya Kati
Ghaith al-Omari, Taasisi ya Washington alisema: “Hamas inasema kusababisha matatizo ya ndani katika misingi ya vitisho, lakini pia kuna khofu kuwa Jordan huenda ikawa ndiyo eneo la mashambulizi kwa Israel. Mambo yote haya yatakuwa na athari kubwa na vitisho kwa utulivu a Jordan na pengine kuwepo kwake.”
Al-Omari amesema mpango wa Trump unaondoa motisha ya Hamas kuendeleza sitisho la mapigano. Jumatatu, Marekani kundi ambalo imelitaja ni la kigaidi lilitishia kuchelewesha mpango ujao wa kuwaachia mateka, wakidai Israel imekiuka sitisho la mapigano.
Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjmani Netanyahu walijibu kuhusu hatua hiyo.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israeli anaeleza: “Uamuzi nimeupitisha kwa kauli moja katika Baraza la Mawaziri nao ni huu: kama Hamas haiwarejeshi mateka wetu ifikapo Jumamosi mchana, sitisho la mapigano litakwisha na IDF waterejesha kwenye mapignao mpaka Hamas ishindwe kabisa.”
Israel itaikabidhi Gaza kwa Marekani baada ya vita, Trump amesema.
Rais Donald Trump amesema kuwa: “Hatutanunua chochote. Tutakuwa kuwa nacho, na tutakiwekwa, na tutahakikisha kuwa kutakuwa na amani na hakutakuwa na tatizo lolote, na hakuna ambaye atatuhoji.”
Maoni mbalimbali yaliyokusanywa na vyanzo vya habari yanaonyesha kuwa wakazi wa Gaza kamwe hawatakubali.
Forum