Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 22:39

Hamas yaachilia mateka zaidi wa Israel


Hamas imewaachilia huru mateka wengine watatu wa Israel, Jumamosi kama sehemu ya makubaliano tete ya kusitisha mapigano, hata wakati Rais wa Marekani, Donald Trump, anaendelea kuendeleza mpango wake wa kumiliki Ukanda wa Gaza.

Haya ni mabadilishano ya tano toka kusitishwa kwa mapigano kati ya Israel na Hamas kuanza kutekelezwa mwezi uliopita. Eli Sharabi, 52 na Ohad Ben Ami, 56 wote walichukuliwa mateka Kibbutz Beeri, shamba la jumuiya, huku Or Levy, 34, alitekwa katika tamasha la muziki la Nova wakati wa shambulizi dhidi ya Israeli, Oktoba 7, 2023.

Kwa upande wake, Israel inatazamiwa kuwaachia huru wafungwa 183 wa Kipalestina baadaye Jumamosi.

Wakati wa awamu ya kwanza ya usitishaji vita, unaotarajiwa kudumu kwa wiki sita, Hamas itawaachia hatua kwa hatua mateka 33 wa Israel kwa kubadilishana na mamia ya wafungwa wa Kipalestina.

Mateka 13 wa Israel na wafanyakazi watano wa Thailand wamesha achiliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG