Rais wa Marekani Donald Trump amerudia tena ahadi yake ya kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza wakati shinikizo likiongezeka kwa Israel na Hamas kuongeza muda wa makubaliano ya kusitisha mapigano zaidi ya ilivyokua katika awamu ya awali.
Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema njaa imeepushwa kwa kiasi kikubwa huku zaidi ya malori 12,600 ya misaada yakiingia katika ukanda huo tangu kuanza kwa usitishaji mapigano. Lakini ikiwa makubaliano hayo hayataongezwa muda kitisho cha njaa kinaweza kurudi, alisema.
Hali bado ni mbaya na watu bado wana njaa, mkuu wa masuala ya kibinadamu Tom Fletcher, ameliambia shirika la habari la Associated Press baada ya ziara ya siku mbili huko Gaza. “Kama usitishaji mapigano utashindikana, ikiwa usitishaji mapigano utakosekana, basi haraka sana hali hizo kama vile njaa zitarudi tena”.
Akiwa katika ndege ya Air Force One akielekea kwenye Super Bowl, Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa anapoteza uvumilivu na hali hiyo baada ya kuona mateka waliotekwa nyara na Hamas wakiachiwa huku wakiwa katika hali dhaifu.
Forum