Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:57

Mmoja auwawa na wengine zaidi ya 200 wakamatwa Kenya


Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga (katikati) akizungumza na wafuasi wake katika kitongoji cha Mathare huko Nairobi mnamo Machi 20, 2023. Picha na YASUYOSHI CHIBA/AFP.
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga (katikati) akizungumza na wafuasi wake katika kitongoji cha Mathare huko Nairobi mnamo Machi 20, 2023. Picha na YASUYOSHI CHIBA/AFP.

Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya ameuawa na zaidi ya watu 200 wamekamatwa wakati wa maandamano yaliyokuwa yakiipinga serikali ya rais William Ruto kuhusu kupanda kwa gharama za maisha, maandamano yaliyofanyika katika maeneo mbalimbali nchini Kenya siku ya Jumatatu, polisi walisema.

Mwanafunzi huyo William Mayange alikuwa ni miongoni mwa waandamanaji wa chuo hicho waliovamia kituo cha polisi na kusababisha maafisa wa polisi kutumia risasi kuwatawanya.

Katika mapambano hayo, polisi walifyatua risasi ambayo ilimpiga shingoni mwanafunzi huyo na kufariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya Coptic, Kisumu. Kulingana na taarifa ya Inspekta mkuu wa polisi nchini Kenya Japheth Koome.

Waandamanaji wengine waliingia katika barabara za mji mkuu wa Nairobi, na miji mingine kadhaa kuitikia wito kutoka kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Baadhi ya waandamanaji hao waliwasha moto mitaani na kuwarushia mawe polisi. Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi na kuwarushia maji yanayowasha waandamanaji hao ukiwemo msafara wa Odinga aliyekuwa akiwahutubia wafuasi wake kutoka kwenye paa la kwenye gari yake.

Polisi walisema maafisa 24 walijeruhiwa katika mapambano hayo. Lakini hawakutoa idadi ya waandamanaji waliojeruhiwa. "Mapambano hayo ya siku nzima yaliyoshuhudiwa jana huko Nairobi na kisumu hayakuwa na msingi zaidi ya kufanya ghasia dhidi ya polisi na kuhujumu uchumi,” walisema polisi katika taarifa ya Jumanne.

Wafuasi wakimshangilia Raila Odinga Machi 20, 2023. Picha na YASUYOSHI CHIBA/AFP.
Wafuasi wakimshangilia Raila Odinga Machi 20, 2023. Picha na YASUYOSHI CHIBA/AFP.

Wakati akiitisha maandamano, Odinga, mwenye umri wa miaka 78, alielezea bei za juu za vyakula vikuu kama vile a unga wa mahindi, ambao umesababisha mfumuko wa bei kuwa juu.
Odinga pia alimshutumu Ruto kwa udanganyifu wa kura wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana. Ikiwa ni mara ya tano mfululizo kwa Odinga kugombea nafasi urais nchini humo alikuwa mshindi wa pili. Odinga alipinga matokeo hayo katika mahakama ya juu ambayo iliidhinisha ushindi wa Ruto.

Jumanne Odinga aliongeza wito wake wa kutaka maandamano yafanyike mara mbili kwa wiki, na kuzitaja siku za Jumatatu na Alhamisi kuwa siku za maandamano kuanzia Machi 27.

Wabunge wanne walikuwa ni miongoni mwa waliokamatwa wakati wa maandamano, wakiwemo viongozi wa kundi la Odinga katika mabaraza yote mawili ya bunge.

Wabunge hao waliachiwa kwa dhamana na watafikishwa mahakamani siku ya Alhamisi kujibu mashtaka ya mkusanyiko usio halali, wakili wao, Danstan Omari, aliliambia shirika la habari la Reuters.

XS
SM
MD
LG