Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 13:43

Kenya: Watu 22 wakamatwa huku maandamano yakigeuka ghasia katika baadhi ya maeneo


Maandamano Kenya.
Maandamano Kenya.

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya walitumia gesi ya kutoa machozi Jumatatu kuwatawanya waandamanaji waliokusanyika mjini Nairobi, na kwingineko nchini, kwa maandamano yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga na wenzake wa muungano wa kisiasa wa Azimio la Umoja - One Kenya.

Maandamano hayo yaliitishwa kupinga kupanda kwa gharama ya maisha, kumtaka Rais William Ruto na utawala wake kuondoka mamlakani, na kupinga mchakato unaoendelea, wa uteuzi wa makamishna wa tume ya uchaguzi na mpipaka, kati ya mengine.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba angalau watu 22, wakiwemo wabunge, walikamatwa kwa kushiriki maandamano hayo, ambao yaliharamishwa na polisi jana Jumapili.

Waandamanaji pia waliwarushia mawe polisi wa kupambana na ghasia nje ya ofisi za serikali katika mji mkuu.

"Tutakuwa hapa hadi gesi ya kutoa machozi imalizike," mwandamanaji mmoja, Markings Nyamweya, 27, aliliambia shirika la habari la AFP.

Katika sehemu moja ya kitongoji duni kikubwa cha Nairobi cha Kibera, waandamanaji pia walichoma matairi, waandishi wa habari wa AFP walisema.

"Ninataka Wakenya wajitokeze kwa wingi na waonyeshe kutofurahishwa na kile kinachotokea katika nchi yetu," Odinga, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwaka jana dhidi ya Ruto, aliwaambia wafuasi wake Jumapili.

Wakenya wanateseka kutokana na kupanda kwa bei ya mahitaji ya kimsingi, pamoja na kushuka kwathamani ya shilingi dhidi ya dola ya Marekani na ukame ulioweka rekodi, kuwaacha mamilioni ya watu njaa.

"Tulikuja hapa kwa amani lakini walitupiga mabomu ya machozi," alisema Charles Oduor, 21. "Wanatudanganya kila siku. Uko wapi unga wa bei nafuu wa mahindi walioahidi? Ajira za vijana walioahidi ziko wapi? Wanachofanya ni kuajiri tu. marafiki zao."

Mkuu wa polisi wa Nairobi Adamson Bungei alisema Jumapili kwamba polisi walipokea maombi ya kufanya maandamano mawili mwishoni mwa Jumamosi na mapema Jumapili, wakati kwa kawaida notisi ya siku tatu inahitajika kwa mikutano ya hadhara.

"Kwa usalama wa umma, hakuna kibali kilichotolewa," alisema.

XS
SM
MD
LG