Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 08:44

Uhaba wa mafuta Kenya changamoto kwa boda boda


Pikipiki ikiwa imebeba waandamanaji mjini Nairobi Kenya, tarehe 6, Juni 2016. Picha na AP/Ben Curtis.
Pikipiki ikiwa imebeba waandamanaji mjini Nairobi Kenya, tarehe 6, Juni 2016. Picha na AP/Ben Curtis.

Uhaba na ongezeko la bei ya mafuta nchini Kenya unasababisha changamoto ya ajira kwa vijana wanaotoa huduma za usafiri wa pikipiki maarufu kama “boda boda”.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika kwa njia ya simu, baadhi yao walisema uhaba wa mafuta unawafanya wanunue mafuta kwa bei ya juu wakati wateja wanashindwa kumudu kiwango kikubwa cha nauli wanachotoza, hivyo kusababisha changamoto katika uendeshaji wa biashara hiyo ya bodaboda inayotoa ajira kwa vijana wengi nchini Kenya.

James Mwangi ni mwendesha bodaboda katika jiji la Nairobi alisema “unapomtajia mteja bei ya usafiri, mnaanza kubishana, halafu anasema hana uwezo wa kulipa kiwango hicho”

“Kwa kuwa gharama za usafiri zimepanda, wateja wanatembea kwa miguu kwa hiyo tunakosa wateja” aliongeza Paul Kuja ambaye pia hutoa huduma hizo za usafiri katika jiji la Nairobi.

Waandesha bodaboda hao wamesema kuwa wakati mwingine wanalazimika kuziegesha pikipiki zao majumbani, na kutafuta mbinu nyingine zitakazowawezesha kujikimu kimaisha na kumudu ongezeko la gharama za maisha lililosababishwa na mfumuko wa bei.

Mchambuzi wa masuala ya uchumi wa Kenya Bravious Kahyoza, amelielezea suala la uhaba wa mafuta nchini Kenya limetokana na upungufu wa fedha za kigeni, tatizo ambalo limesababishwa na madeni yanayotokana na ukopaji mkubwa kutoka nje na janga la COVID ambalo lilivuruga mpangilio wa hifadhi ya fedha (reserve) ambapo kiwango kikubwa cha pesa hizo zingetumika katika uingizaji wa mafuta nchini.

Kwa sasa Kenya inakabiliwa na upungufu wa fedha za kigeni ambazo zinatumika katika uagizaji wa bidhaa muhimu zikiwemo vifaa vinavyotumika kutegenezea miundo mbinu. Uagizaji wa mafuta nchini Kenya unagharimu zaidi ya asilimia 60 ya hifadhi ya fedha (reserve), “hii ina maana kwamba kama hakuna fedha za kutosha zilizohifadhiwa, Kenya haina uwezo wa kuagiza mafuta.

XS
SM
MD
LG