Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 19:29

Misri yasema eneo la Mediterranean lina gesi ya kutosheleza mahitaji ya Ulaya


 Waziri wa Nishati wa Misri Tarek El-Molla,
Waziri wa Nishati wa Misri Tarek El-Molla,

Waziri wa Nishati wa Misri anasema usambazaji wa gesi katika eneo la Mediterranean kwa hakika lina gesi ya kutosha kukidhi mahitaji ya Ulaya kama uwekezaji utafanyika ili kuvitumia kikamilifu vinu vya katika eneo hilo.

Televisheni za Misri ziliripoti Jumamosi kwamba Rais wa Cyprus Nicos Anastasiades aliishukuru Misri kwa juhudi zake za kufanya uratibu wa pamoja wa kutumia gesi ya asili iliyopo chini ya bahari na hivyo kikao maalum cha East Mediterranean Gas kilifanyika mwezi Juni.

Vyombo vya habari vya Kiarabu pia viliripoti Jumamosi kwamba Waziri wa Nishati wa Misri, Tarek el Molla, ambaye alihudhuria kikao cha siku moja ambacho kilihudhuriwa na mataifa kadhaa huko Cyprus siku ya Ijumaa, alisema kwamba usambazaji wa gesi katika eneo la Mashariki mwa Meditarranean itakuwa kile ambacho kinaitwa “muokoaji wa maisha kwa Ulaya wakati wa shida kubwa,” na “huenda hatimaye wakakidhi mahitaji ya gesi ya Ulaya kama uwekekezaji sahihi utafanywa.”

Rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades
Rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades

Misri imekuwa mkosoaji mkali katika siku zilizopiwa kwa taasisi za Ulaya na za kimataifa za fedha kwa kutokuwa tayari au hawana hamasa kuhusu kufanya uwekezaji katika eneo hilo kwenye vinu vya mafuta ili kushirikiana mzigo katika uzalishaji wa gesi katika vinu kadhaa vya chini ya bahari, ambapo mara kwa mara vinakuwa na gharama kubwa.

Mwana sosholojia wa kisiasa raia wa Misri, Said Sadek ameiambia kwamba mzozo wa sasa wa kimataifa unatokana na vita kati ya Russia na Ukraine ambavyo hatimaye huenda vikaisha “kama gesi ya Russia itasafirishwa tena kupitia bomba la mafuta kwenda Ulaya, itaifanya baashi ya gesi ya Mashariki mwa Mediterranean isiwe na faida kubwa.”

Sadek ameelezea kwamba idadi ya vinu vya mafuta vimekumbwa na matatizo yanayohusishwa na uhasimu na mizozo kati ya Misri na Uturuki – juu ya vinu vilivyopo karibu na Libya na Ugiriki – na Uturuki juu ya vinu ambavyo viko katika maji ya Cyprus, na katika vinu kati ya Ugiriki na Uturuki.

“Mediterranean imejaa gesi – ya kutosha kuiuza nje, lakini tatizo ni mapambano, hasa tatizo na Lbya ni lenye mkanganyiko na litachukua muda, na kwenye kinu cha Cana huko Lebanon hakiko tayari. Uturuki inatakaz ipewe kipande cha keki na walijaribu kuinyanyasa Ugiriki kwa njia mbali mbali,” anasema Sadek.

Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Sadek ameelzea kwamba Rais wa Russia Vladimir Putin aliripotiwa kumwambia mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, wakati alipoitembelea Moscow hivi karibuni, kwamba ni vyema aongeze bomba la gesi la TurkStream ambalo liwe ni kutoka Russia hadi Uturuki kupitia mashariki mwa Ulaya,” Sadek aliongeza kwamba hatua kama hiyo “iliizikasirisha nchi kadhaa na huenda ikachukua miaka kadhaa kufanyika kwa. Hilo, kwa njia yoyote ile.”

Mchambulizi wa masuala ya nishati mwenye makao yake nchini Marekani Paul Sullivan anakubaliana na Sadek, alieleza kwmaba “kuna gesi nyingi huko mashariki mwa Meditarranea lakini itachukua muda mrefu sana kuwa tayari kwenye vinu na miundo mbinu ya usafiri ili kuifikisha gesi hiyo sokoni pia ni mtihani.” Alisistiza kwamba “kadri muda unavyokwenda vinu vya gesi huko Medittaranean Mashariki huenda vikwa na gesi nyingi ya kuipeleka Ulaya na sehemu nyingine.”

“Kuwekeza katika vinu hivi,” aliongezea, “ni pamoja na fedha na kuchukua hatari za kisiasa na nyingine,” pia.

XS
SM
MD
LG