Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 08:48

Rais wa Gabon aomba Afrika kuweka mikakati ya kulinda mazingira


Rais wa Gabon Ali Bongo Ondimba.

Mataifa ya Afrika yameombwa yaweke mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yanatishia miji mikuu barani humo.

Hayo yamesemwa na Rais wa Gabon Ali Bongo kwenye kongamano la tatu la hali ya hewa la Afrika kwenye mji mkuu wa taifa hilo wa Libreville. Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Bongo ameongeza kusema kwamba maafisa wa Afrika pamoja na wataalam wengine wanahitaji kupasa sauti zao wakati wa kongamano la 27 la Umoja wa Mataifa litakalofanyika Misri mwezi Novemba.

Kongamano la wiki moja la Gabon limewaleta pamoja zaidi ya maafisa 1,000 wa serikali pamoja na wadau wengine wa mabadiliko ya hali ya hewa. Kongamano hilo linafanyika wakati Afrika inakabiliana na majanga kadhaa ya mazingira kama vile ukame kwenye baadhi ya mataifa ya Afrika mashariki na pembe ya Afrika, dhoruba ya mchanga pamoja na joto kupita kiasi kwenye eneo la Sahel pamoja na mafuriko na vimbunga vingine katikati , kusini na magharibi mwa Afrika.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG