Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 05:20

Misri: Muslim Brotherhood wakataa kushirikiana harakati za kutafuta madaraka


Wanaharakati wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, Misri.
Wanaharakati wa vuguvugu la Muslim Brotherhood, Misri.

Vuguvugu lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood nchini Misri, halitashirikiana na mamlaka ambayo iliiondoa katika serikali miaka tisa iliyopita, katika kuanzisha mapambano mapya ya kutafuta madaraka, ingawa bado lina uungwaji mkono mkubwa, kaimu kiongozi wake amesema.

Vuguvugu hilo ambalo kwa wakati mmoja lilionekana kuwa na nguvu mno, lilishinda uchaguzi wa kwanza, huru, wa rais, nchini Misri mnamo mwaka wa 2012, lakini lilipinduliwa na jeshi mwaka mmoja baadaye, kufuatia maandamano makubwa ya kupinga utawala wake, na limevumilia ukandamizaji mkali wa mamlaka tangu wakati huo, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Viongozi wake wengi na maelfu ya wafuasi wake, wako jela au wametoroka Misri, na kundi hilo limeondolewa kwenye mazungumzo ya kisiasa yatakayozinduliwa hivi karibuni na Rais Abdel Fattah al-Sisi, ambaye kama mkuu wa jeshi, aliondoa utawala wa vuguvugu hilo mnamo mwaka mwaka wa 2013.

Cairo imeliorodhesha kundi la Brotherhood kama shirika la kigaidi, lakini kaimu kiongozi Ibrahim. Munir, alisisitiza madai yamuda mrefu ya kundi hilo, kwamba linapinga ghasia.

XS
SM
MD
LG