Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 13:56

Misri yahukumu kifo wanachama wa Muslim Brotherhood


Kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohamed Badie akiwa kizuizini kwenye picha ya awali.

Mahakama moja ya Misri alhamisi imewahukumu kifo wafuasi 24 wa chama cha Muslim Brotherhood, kwa kuwauwa maafisa wa polisi katika matukio mawili tofauti.

Mahakama ya uhalifu ya Damanhour, kaskazini mwa mji mkuu Cairo, imelikuta kundi la watu hao na hatia kwa makosa kadhaa ya uhalifu, ikiwemo madai ya kushambulia kwa bomu basi lililokua linasafirisha maafisa wa polisi katika mkoa wa pwani wa Beheira mwaka 2015. Shambulio hilo liliuwa maafisa watatu wa polisi na kujeruhi wengine wengi.

Washtakiwa wanane kati ya 24 walihukumiwa bila kuwepo. Hukumu ya kifo kwa raia waliokutwa na hatia nchini Misri, inatekelezwa kwa kunyongwa. Hukumu hizo zinaweza kukatiwa rufaa, chanzo cha mahakama kimeongeza.

Misri ililipiga marufuku kundi hilo la kiislamu mwaka 2013 kufuatia kuondolewa madarakani na jeshi kwa rais wa zamani Mohamed Morsi.Tangu aongoze jeshi na kuwa rais, Abdel Fattah al Sisi alifanya msako mkali kwa chama cha Muslim Brotherhood, na maelfu ya wafuasi wake walifungwa jela.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG