Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:25

Nchi za Afrika kutumia mazungumzo ya ya COP27 Misri kutetea msimamo wa pamoja wa nishati


Mhandisi wa mzaliwa wa Misri na raia wa Ujerumani Hani Azer, msimamizi wa Kituo Kikuu cha Treni cha Berlin, anashiriki katika mpango wa "Nile Cleanup" kukusanya taka za plastiki kwenye ukingo wa Mto Nile huko Cairo, Misri, Alhamisi, Septemba 29, 2022 (Picha ya AP/Amr Nabil)
Mhandisi wa mzaliwa wa Misri na raia wa Ujerumani Hani Azer, msimamizi wa Kituo Kikuu cha Treni cha Berlin, anashiriki katika mpango wa "Nile Cleanup" kukusanya taka za plastiki kwenye ukingo wa Mto Nile huko Cairo, Misri, Alhamisi, Septemba 29, 2022 (Picha ya AP/Amr Nabil)

Nchi za Afrika zitatumia mazungumzo ya hali ya hewa ya COP27 nchini Misri mwezi ujao kutetea msimamo wa pamoja wa nishati ambao unapelekea  nishati ya mafuta ambayo ni muhimu katika kupanua uchumi na upatikanaji wa umeme, afisa mkuu wa nishati barani Afrika  alisema Jumanne.

Msimamo wa Kiafrika, uliokosolewa na mashirika ya mazingira, unaweza kufunika mazungumzo ya hali ya hewa ya kimataifa huko Sharm El-Sheikh ya kutaka kuendeleza mkutano uliopita wa Glasgow na kufikia malengo ya ufadhili wa mataifa tajiri kwa nchi masikini ambazo ziko nyuma sana katika kutimiza ahadi ya dola bilioni 100 zilizoahidiwa kwa mwaka ikufikia mwaka 2020.

Tunatambua kuwa baadhi ya nchi zinaweza kutumia nishati ya mbadala ya mabaki ya wanyama na mimea kwa sasa, lakini si suluhu moja inayofaa kwa wote, alisema Amani Abou-Zeid, Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) wa Miundombinu na Nishati.

Sio wakati wa kuwatenga, lakini ni wakati wa kuandaa suluhisho kwa muktadha,aliiambia Reuters kando ya mkutano wa mafuta na gesi.

Utafiti wa kiufundi wa AU uliohudhuriwa na nchi 45 za Afrika tarehe 16 Juni uliopatikana na Reuters ulieleza kuwa mafuta na makaa ya mawe yatachukua jukumu muhimu katika kupanua upatikanaji wa nishati ya kisasa katika muda mfupi hadi muda wa kati.

XS
SM
MD
LG