Vifo vingi vimetokea katika miji miwili mikubwa ya Lilongwe and na Blantyre ambako wanafunzi hivi karibuni walirejea kwenye masomo baada ya shule kuchelewa kufunguliwa ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Chiponda aliwataka watu kuchukua tahadhari zaidi wakati wakiishughulikia miili ya waliofariki kwa kipindupindu kabla ya mazishi. “Watu wanaokufa kwa kipindupindu wanaweza kuoshwa na wanafamilia ambao baadaye huandaa chakula cha mazishi... kawaida milipuko ya kipindupindu hufuatia karamu hizi” amesema.
Waziri amewataka watu kutumia njia sahihi za kuzuia maambukizi ikiwemo utumiaji wa chlorini na mifuko ya plastiki ya kuhifadhia miili ya marehemu.
Kipindupindu mara kwa mara huikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika wakati wa msimu wa mvua kuanzia Novemba hadi Machi, Lakini kumekuwa na ongezeko kubwa la uchafuzi usio wa kawaida wakati na baada ya msimu wa sikukuu. Kwa kawaida idadi ya vifo kwa mwaka ni karibu 100.
“Jumla ya maambukizi na vifo yaliyothibitishwa tangu kuanza kwa mlipuko, ni maambukizi 30,621 na vifo 1,002 vilivyothibitishwa, huku vifo vikiwa ni asilimia 3.27,” Chiponda alisema.
Maafisa wa afya wamesema wiki iliyopita baadhi ya zahanati nchini humo zilipokea dozi milioni 2.7 za kipindupindu kwa mujibu wa program ya Shirika la Afya Duniani, tayari kuna upungufu.
Wizara ya afya ilikataa kutoa maoni juu ya idadi ya chanjo zilizoko wakati shirika la habari la Reuters lilipowasiliana nao.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.