Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:41

Haiti yaanza kutoa chanjo dhidi ya kipindupindu nyumba hadi nyumba Port au Prince


Dkt Carissa F. Etienne (Katikati) Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan American -PAHO
Dkt Carissa F. Etienne (Katikati) Mkurugenzi wa Taasisi ya Pan American -PAHO

Kampeni ya chanjo dhidi ya kipindupindu imeanza nchini Haiti huku maafisa wa afya wakipita nyumba kwa nyumba katika baadhi ya ujirani katika mji mkuu wa Port au Prince.

Taasisi ya Afya ya Pan American – PAHO, ilituma kiasi cha dozi za chanjo milioni 1.17 za kunywa mapema mwezi Desemba wakati kesi zikiendelea kuongezeka nchini humo.

Kampeni ya awali ililenga watu walio na umri kati ya mwaka mmoja katika maeneo ya Cite Soleil, Delmas, Tabarre, Carrefour na Port au Prince katika idara ya Quest maeneo ambayo ndiyo yenye kesi nyingi za kipindupindu kuripotiwa hadi hivi sasa.

Jumanne, wafanyakazi wa afya walipita katika mitaa myembamba kwenye ujirani wa Canneau katikati ya Port au Prince ambako kesi kadhaa za kipindupindu pia zimeripotiwa.

Kusambaa kwa kipindupindu kumekuja wakati mji mkuu ukiathiriwa na kusambaa kwa ghasia zinazofanywa na magenge yenye silaha na kuchukua udhibiti wa maeneo kadhaa katika mji.

XS
SM
MD
LG