Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:53

Uhalifu umeongezeka Haiti kutokana na hali ngumu ya maisha, 89 wameuawa


Ndege ikiteketea kwa moto baada ya waandamaji kuiwasha moto nchini Haiti.
Ndege ikiteketea kwa moto baada ya waandamaji kuiwasha moto nchini Haiti.

Watu 89 wamefariki kutokana na mashambulizi ya makundi ya uhalifu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince kufuatia kuongezeka kwa gharama ya maisha na ambayo imepelekea kutokea maandamano.

Kundi la kutetea haki za binadamu limesema kwamba watu wengine 16 hawajulikani walipo.

Hali ya usalama imeendelea kuharibika nchini Haiti kutokana na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu na ukosedu wa mafuta.

Machafuko yalianza July 7 kufuatia makabiliano kati ya makundi mawili yanayohasimiana katika mtaa wa Cite Soleil, karibu na Port-au-Prince, wenye kiwango cha juu cha umaskini, na ulio na idadi kubwa ya watu.

Mashambulizi ya bunduki yameongezeka katika mtaa huo, huku polisi ambao hawana vifaa vya kutosha wakishindwa kuingilia kati.

Mashirika ya kimataifa ya haki za kibinadamu yamekuwa na wakati mgumu kuhakikisha kwamba chakula na dawa vinawafikia waathiriwa.

Maelfu ya watu wanaoishi katika mtaa huo wa mabanda wamelazimika kujificha katika nyumba zao kutokana na ukosefu wa usalama.

Wamekosa chakula, wala maji safi.

Watu kadhaa wamefariki kutokana na majeraha ya risasi zilizopigwa kiholela.

XS
SM
MD
LG