Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 29, 2024 Local time: 12:01

Marekani kupitia maombi ya Haiti ya msaada


Marekani imesema inapitia maombi ya Haiti ya msaada wa usalama katika kipindi hiki kuna hali ya kutokuwa na usalama na mahitaji makubwa ya msaada wa kibinadamu.

Mwanadiplomasia wa juu katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani kwa ukanda wa magharibi, Brian Nichols, anaelekea katika taifa hilo kisiwa cha Caribbean leo hii kufanya tathimini ya hali ya mambo.

Makundi yenye silaha kali yanadhibiti doria katika mji mkuu wa Port-au-Prince na wamezuia njia ya kuelekea katika kituo kikubwa cha mafuta toka katikati ya mwezni Septemba.

Hali hii imefanya hali kuwa mbaya zaidi katika mazingira ambayo tayari yameshakuwa mabaya kwa hali ya kibinadamu, kuathiriwa kwa upatikanaji wa umeme, maji safi, ukusanyaji wa uchafu, na namna ya hospitali kufanyakazi.

XS
SM
MD
LG