Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 20:24

Watu saba wafariki kwa ugonjwa kipindupindu Haiti


Mtoto aliyekutwa na ugonjwa wa kipindupindu akipata matibabu, Jumanne, Oktoba 11, 2016, huko Anse D'Hainault, Haiti.
Mtoto aliyekutwa na ugonjwa wa kipindupindu akipata matibabu, Jumanne, Oktoba 11, 2016, huko Anse D'Hainault, Haiti.

Haiti siku ya Jumapili imesema takriban watu saba wamefariki dunia kwa ugonjwa kipindupindu katika kurudi kwa mshangao kwa ugonjwa huo ambao unakuja wakati taifa hilo limegubikwa na kizuizi cha magenge ambacho kimesababisha uhaba wa mafuta na maji safi ya kunywa.

Ugonjwa huo uliua takriban watu 10,000 kupitia mlipuko wa mwaka 2010 ambao umelaumiwa kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa. Shirika la Afya la Pan American mwaka 2020 lilisema Haiti ilikaa mwaka mmoja bila kesi iliyothibitishwa ya kipindupindu.

Kulingana na taarifa tulizonazo, idadi ya vifo ni takriban 7 hadi 8," alisema na kuongeza kuwa maafisa walikuwa wakihangaika kupata taarifa kutoka hospitalini. "Kulikuwa na kifo kimoja wakati wa mchana leo."waliongeza.

Wizara ya Afya hapo awali ilithibitisha kisa kimoja katika eneo la Port-au-Prince na kwamba kulikuwa na visa vinavyoshukiwa katika mji wa Cite Soleil nje ya mji mkuu, ambao ulikuwa eneo la vita vikali vya magenge mwezi Julai.

Tangu mwezi uliopita, magenge yamekuwa yakizuia bandari kuu ya mafuta nchini humo kupinga tangazo la Septemba la kupanda kwa bei ya mafuta. Hospitali nyingi zimefunga au kupunguza shughuli kwa kukosa mafuta ya jenereta.

Usafiri wa kawaida kwa sasa haupatikani kwa raia wengi.

XS
SM
MD
LG