Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 01:21

WHO yasema maambukizo ya kipindupindu yanaongezeka katika sehemu nyingi za dunia


WHO yasema maambukizo ya kipindupindu yanaongezeka katika sehemu nyingi za dunia
please wait

No media source currently available

0:00 0:15:00 0:00

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema tangu Januari mwaka 2022, takriban nchi 29 zimeripoti milipuko mipya ikiwemo nchi 13 ambazo hazikuwa na ugonjwa huo mwaka ulotangulia wa 2021.

Kipindupindu ni maambukizi mabaya yanayosababisha kuharisha ambayo yanaweza pia kusababisha upungufu wa maji mwilini. Huenezwa kwa kula chakula au maji yenye bakteria wa kipindupindu. Maafisa wa afya nchini Cameroon wanasema mamia kadhaa ya visa vya kipindupindu vimegunduliwa katika mpaka wa kaskazini mwa nchi hiyo na Nigeria, huku watu wasiopungua 17 wamefariki. Mlipuko nchini Malawi ambao umesambaa katika wilaya 22 umesababisha vifo vya zaidi ya watu 100. Mashirika ya misaada yanaongeza tahadhari juu ya kuongezeka kwa mlipuko nchini Haiti, huku zaidi ya watu 600 wakishukiwa au kuthibitishwa katika eneo linalozunguka mji mkuu wa Port-au-Prince. Ugonjwa huu umeambukiza na kuua watu katika nchi kama Syria na Lebanon.

Kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa kipindupindu duniani, shirika la afya duniani (WHO) limeripoti uhaba wa dozi za chanjo ya kipindupindu, na kulazimisha mabadiliko ya muda katika mkakati wa dozi moja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG