Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:27

Cameroon: Rais Biya aadhimisha miaka 40 madarakani


Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Cameroon Paul Biya.

Rais Paul Biya wa Cameroon anaadhimisha miaka 40 madarakani huku maswali mengi yakiulizwa kuhusu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 89.

Biya hajaonekana hadharani tangu Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kutembelea taifa hilo la Afrika ya Kati mwezi Julai.

Amri za kiutendahji na picha za Biya akipokea wanadiplomasia mbalimbali huwekwa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii ya rais Biya.

Maelfu walihudhuria sherehe mjini Douala Jumapili lakini Biya hakuwepo. Baadhi ya watu wanafikiri mwanaye Rais Biya anajiandaa kuwa mrithi wake.

Kuna hofu kwamba mwisho wa muda wa rais Biya unaweza kusababisha kuzuka kwa machafuko.

Wakosoaji wanaulaumu utawala wake kwa kuwezesha kukita mizizi ya ufisadi nchini humo.

Biya ni mmoja wa viongozi waliotawala kwa muda mrefu zaidi barani Afrika.

XS
SM
MD
LG