Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 19:52

UNICEF yaisaidia Malawi vifaa kwa kupambana na kipindupindu


Wafanyakazi wa afaya wakitibu wagonjwa wa kipindupindu , Malawi
Wafanyakazi wa afaya wakitibu wagonjwa wa kipindupindu , Malawi

Vifaa hivyo ni pamoja na seti za Acute Watery Diarrhea aina ya tiba inayosaidia kuongeza maji mwilini, mahema ya utendaji wa hali ya juu, dawa aina ya Antibiotics na nyinginezo na vifaa vya tiba.

Mchango huo unafuatia tangazo la rais wa Malawi Lazarus Chakwera mwezi Decemba kuhusu huduma ya dharura na msaada wa ndani na wa kimataifa katika kupambana na mlipuko wa kipindupindu.

Rudolf Schwenk ni mwakilishi wa UNICEF nchini Malawi anasema wataendelea kusaidia wizara ya afya kwa ajili ya kukabiliana na kipindupindu , na wanaheshimu juhudi za bila kuchoka zinazofanywa na wafanyakazi wa huduma za afya walioko mstari wa mbele kwa ajili ya kudhibiti kuenea vitisho na mlipuko na kuhakikisha afya bora kwa watoto.

Takwimu kutoka taasisi ya afya ya taifa ya Malawi inasema kuwa ugonjwa huo umeuwa watu 773 ikiwemo watoto 104 na kusababisha kesi za kipindupindu zaidi ya 23,000 tangu mlipuko huo kutokea.

XS
SM
MD
LG