Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 00:07

Shule katika miji miwili mikubwa ya Malawi zitaendelea kufungwa kutokana na mlipuko wa kipindupindu


Wakazi katika mji wa Malawi, Blantyre wakijianda kupata chanjo dhidi ya kipindupindu, Novemba 16, 2022. Picha ya Reuters
Wakazi katika mji wa Malawi, Blantyre wakijianda kupata chanjo dhidi ya kipindupindu, Novemba 16, 2022. Picha ya Reuters

Shule katika miji miwili mikubwa nchini Malawi zitaendelea kufungwa hadi itakapotangazwa baadaye kutokana na mlipuko mbaya sana wa kipindupindu, serikali ilisema Jumatatu.

Wanafunzi walitarajiwa kurejea shule leo Jumanne baada ya likizo ya siku kuu.

Lakini wizara ya afya imesema kuanza kwa muhula wa masomo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika mji mkuu Lilongwe na mji wa kusini wa Blantyre kutacheleweshwa kwa angalau wiki mbili.

Waziri wa afya Khumbize Chiponda alisema katika taarifa kwamba kuakhirishwa kwa masomo kunatokana na ongezeko la hivi karibuni na linaloendelea la idadi ya visa vya kipindupindu na vifo.

Aliongeza kuwa mamlaka “inasikitishwa na usumbufu wowote uliosababishwa na hatua ya dakika za mwisho iliyochukuliwa kwa ajili ya usalama wa wanafunzi.”

Taifa hilo maskini la kusini mwa Afrika limerekodi visa 18,000 vya kipindupindu na vifo 595 tangu mwezi Machi kwa kile Umoja wa Mataifa ulisema ni mlipuko mkubwa sana kulikumba taifa hilo katika kipindi cha miaka 10.

Wakati wa mkesha wa mwaka mpya, waziri Chiponda alitoa wito mwingine kwa viongozi wa dini kuwahimiza waumini wao kutafuta matibabu kwa sababu baadhi yao walikuwa wanakwepa kupata huduma kwa misingi ya kidini.

XS
SM
MD
LG